Miujiza Kutoka Mbinguni!
· na Shajara Administrator
Yesu anawakatalia kutimiza ishara waliouliza na anawaacha wakiwa wamesimama na kupakia mashua na kwenda ngambo nyingine ya bahari. Ni hakika kuondoka kwake ni alama ya kuto kupendezwa na mitizamo ya Mafarisayo. Sisi pia mara nyingi tumekuwa watu wakutaka ishara kutoka kwa Mungu, tunasahau ishara ya upendo wa Mungu anaotupa sisi kila siku katika maisha yetu. Imani yetu ndogo iliojazwa na akili na majivuno inatufunga tushindwe kuona miujiza mingi anayotenda Mungu katika maisha yetu. Imani yetu inatudai tubaki tukiwa waaminifu na wazi kwa Mungu, kwani anafunua Upendo wake katika udogo na unyenyenkevu.
Ni mara chache sana tunaweza kufikiria juu ya upendo wa Yesu kwa Mafarisayo. Mara nyingi, tunamfikiria akiwa mkali na kuwalaumu. Lakini kila neno alilokuwa akiwaambia likiwa kali lililenga kuwabadilisha wabadilike, alifanya hivyo kwasababu ya upendo wake. Ilikuwa ni jitihada yake ya kuwatoa katika hali ya tofauti na kuwaleta kwenye neema walio ikataa. Tutafakari, je sisi tupo kama Mafarisayo wanao kataa zawadi ya upendo wa Mungu anayotoa Yesu?
Sala:
Bwana, nisaidie nikupende kwa moyo mkunjufu na upendo mtakatifu. Nisaidie niweze kujuta juu ya dhambi zangu na dhambi za wengine. Nisadie majuto hayo yaweze kunifanya niwe na upendo zaidi na zaidi. Yesu nakuamini wewe.
Amina.
Maoni (3)
Pius Leodigard · 17 Februari 2025
Asante sana ndugu yetu kwa uinjirishaji mzuri .Ni kweli wanadamu tunafuatilia sana ishara kuliko Imani na apo ndipo tunaangukia katika changamoto mbalimbali za kinaisha unashangaa unajikuta wewe ndo huishiwi na matatizo kumbe ni wewe kikimbilia kuamini kwa mwili kiluko kuamini kwa roho Maoni yangu ndo hayo asante

John Jacob · 17 Februari 2025
Amin