Ruka hadi maudhui
Mkatoliki Leo
Tafakari

Kuwa Wazalishaji kwa Ajili ya Ufalme wa Mungu!

· na Shajara Administrator

Masomo ya siku hii Jumatano ya 33 ya Mwaka → Ufu 4:1-11 · Zab 150 · Lk 19:11-28
Mfano wa leo kutoka katika Injili, wakati Mfalme alivyorudi, alihitaji hesabu kutoka kwa kila mtumishi. Kwa njia hii kila mmoja wetu atatoa hesabu ya jinsi tulivyo tumia vizuri talanta na vipiji tulivyopewa na Mungu. Kati ya Wayahudi waliokuwa katika mstari wa Mafarisayo, wao walidhania Mungu kuwa hakimu mkali aliyewatenda kadiri ya faida waliopata kwa kushika sheria. Hali hii iliwajengea watu hofu na wakashindwa kukuwa. Na zaidi sana, iliwafungia hata wao wenyewe kushindwa kufungua mioyo na kukubali hali mpya ya kukutana na Mungu alioleta Bwana wetu Yesu Kristo. Je, wewe na mimi tukoje? Tumetumiaje, au tunatumiaje vipaji alivyotupa Mungu? Je, tutakana uaminifu wake kwetu?

Sala:
Baba, nakushukuru kwa kuni amini mimi na kunipa vipaji na nafasi, yote yaliotoka katika mikono yako. Nisaidie mimi nijifunze kuwa mzalishaji wa kweli kwa ajili ya ufalme wako.
Amina
0 Maoni
WhatsApp Facebook

Maoni (0)

Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.

Ingia utoe maoni