Ruka hadi maudhui
Mkatoliki Leo
Tafakari

Kutembea katika Njia Wasio Safiri Mara kwa Mara!

· na Shajara Administrator

Masomo ya siku hii Kumbukumbu ya Mt. Karoli Borromeo, Askofu → Fil 2:1-4 · Zab 131 · Lk 14:12-14
Somo la Injili la leo linatuangaza sisi kuwanyanyua maskini na wale waliotengwa kama wafuasi wa Kristo. Luka leo anaelezea tukio ambalo Yesu alialikwa na mmoja wa fariso kwa chakula cha jioni. Katika kipindi cha Yesu ilikuwa kawaida watu kuwaalika marafiki, ndugu na jamaa kwa chakula. Hakuna ambaye angeweza kukaa mezani na mtu asiyemfahamu. Walikaa mezani na wale tu walio wafahamu na marafiki. Yesu hafurahishwi na hali hii au utamaduni huu wa watu. Anawaalika kuvunja hali hizo za kualikana watu wa karibu tu, na badala yake wawaalike pia: maskini, viwete, waliotengwa na vipofu. Yesu kwakufanya hivi anatuongoza kwenye Baraka: “Mtabarikiwa kwasababu hawana cha kuwalipa”. Tunapaswa kufanya hivi bila kuwa na mambo binafsi na hofu ya watu ili tuweze kupata Baraka hii. Yesu anaikumbusha jamii pia kuvuka viwango vyao vya kujiwekea mipaka na badala yake kuhubiri Injili ya upendo.

Sala:
Tusaidie Bwana, tufanye ulichosema, hata ikiwa kinaenda kinyume na tamaduni zetu.
Amina.
0 Maoni
WhatsApp Facebook

Maoni (0)

Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.

Ingia utoe maoni