Jumapili. 05 Mei. 2024

Tafakari

Jumatatu, Januari 29, 2024

Jumatatu, januari 29, 2024
JUMA LA 4 LA MWAKA

2 Sam 15:13-14.30;16:5-13
Zab 3:1-7
Mk 5: 1-20.


KUBADILISHWA NA YESU!

Leo tunaona Yesu anakutana na mtu mwenye pepo wachafu wengi. 'Legioni' wa mapepo anatambua nguvu na utakatifu wa Yesu, na anamsihi asiwapeleke nje ya nchi ile. Yesu anawaamuru kwamba wao wamtoke mtu huyo na kwa nguvu ya Neno lake waende kwenye kundi kubwa la nguruwe, kisha nguruwe waliokuwa gengeni wakateremka kwa kasi, na kuzama katika bahari.

Katika injili ya Marko, Legioni (Jeshi) ni ishara ya Roma. Utakatifu wa Yesu na nguvu, itakuwa kwaajili ya kuwakomboa wote waliofungwa na roho ya dhambi. Mabaya hayawezi kusimama dhidi ya Yesu yatashindwa kwa ukweli na mamlaka yake. Uchaguzi ni wetu kuwa huru au la. Wagerasi walimuomba Yesu aondoke katika eneo lao kutokana na hofu ya nguvu zake. Yule aliyekombolewa alikwenda sehemu mbalimbali, kueneza habari njema.

Je! wewe na mimi tukoje? Je! uko tayari kukombolewa au tunataka kumkataa Yesu kama Wagerasi? Mungu ametupa utashi wakutambua mema na mabaya, ni juu yetu kutumia uhuru wetu vizuri kuchagua lililo jema kwa manufaa ya roho zetu. Dhambi ni matokeo mabaya ya matumizi ya uhuru aliotupa Mungu. Mungu kamwe haingilii uhuru wetu, wakati mwingine tunaona mambo mengi mabaya yanatokea tunajiuliza Mungu haoni kweli? Ukweli ni kwamba Mungu anaona lakini kamwe haingilii uhuru wa mwanadamu aliompa anapenda sisi tutumie uhuru wetu vizuri tukijua mabaya na mema, ili tuwe huru kuchagua kati ya hayo mawili. Tuombee neema yake ili tumchague yeye aliye asili ya wema wote.

Sala:
Bwana, ninafurahi katika nguvu zako za Kuu. Ninafurahiai katika ukuu wako na utukufu wako. Nisaidie niweze kuona mara nyingi unapokuwa katika hali mbalimbali ukitenda kazi ndani ya wote walio karibu yangu. Ninapo ona nguvu yako ya kuokoa ikiwa katika kazi, jaza moyo wangu kwa shukrani kwa yote unayotenda. Ninaomba Neno lako na mamlaka yako yafukuze yote yanayo niongoza kwenye dhambi. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni