Jumatatu, Oktoba 09, 2023
Jumatatu, Oktoba 9, 2023
Juma la 27 la Mwaka wa Kanisa
Yon 1: 1-17; 2: 10
Yon 2: 1-3,7 (R) 6;
Lk 10: 25-37.
KUCHUNGUZA UPENDO WETU
Leo katika Injili mwalimu wa sheria anamuuliza Yesu swali ambalo, sisi tungeweza kujiuliza katika maisha yetu ya kila siku. “Bwana, nifanye nini ni urithi Ufalme wa milele?” (Lk 10: 25). Yesu, lakini, tena katika hekima anajibu kwa yale yalioandikwa katika Maandiko: ‘kumpenda Bwana Mungu wako na jirani yako kama nafsi yako’ (rej. Lk 10: 27). Kupenda maana yake ni kujitoa kwa wengine kwa yote tulio nayo na yote jinsi tulivyo. Kujitoa kusikiliza wengine kujitoa kuelewa wengine na kuwa na subira kwa ajili ya wengine. Huo ndio upendo. Upendo huu unakuwa na asili ya Kimungu tunapo ueneza zaidi kwa wale walio tuumiza katika maisha au kwa wengine tusio waona hata macho kwa macho. Upendo unakuwa na Mguso wa Kimungu tunapo toka njee kwenda kuwasaidia hata watu tusio wafahamu. ‘Kama mtu mmoja anateseka, watu wote wanateseka naye, kama mmoja anaheshimiwa, watu wote wanashiriki katika furaha yake’ (1 Cor 12: 26). Hii ndiyo fadhila ya Msamaria mwema.
Ni rahisi kuwa mtu wa kuhukumu na kuwa mkali kwa wengine. Ukisikiliza magazeti au kusikiliza taarifa mbali mbali huwezi kusikia mara nyingi jambo la kumsaidia mtu sana bali mara nyingi ni kuhukumu. Ubinadamu wetu unaonekana mara nyingi kuwa wakali kwa ajili ya wengine. Na wakati ambapo hatuwi wakali tunashawishika kuwa kama makuhani- mlawi katika simulizi hili. Tunashawishika kufunga macho kwa wale ambao wanahitaji msaada wetu. Cha muhimu ni kuonesha huruma na kuuonesha katika hali ya juu. Tutafakari leo, juu ya wito aliokuitia Mungu kukuonesha huruma. Mtakatifu Mama Teresa aliwahi kusema “…kama unapenda mpaka kunakuwa na uchungu, hakuwezi tena kuwa na uchungu bali upendo zaidi”. Huruma ni aina ya upendo ambao mwanzo inaweza kuumiza kwanza lakini mwishoni inaacha upendo mtupu.
Sala:
Bwana, nifanye mimi chombo cha upendo wako na huruma yako. Nisaidie mimi kuonesha huruma pale ambapo ni ngumu katika maisha. Nisaidie nyakati hizo wakati unani badilisha mimi kuwa chombo cha zawadi ya neema yako. Yesu, nakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni