Ruka hadi maudhui
Mkatoliki Leo
Tafakari

Kufungua Mioyo Yetu kwa Yesu

· na Shajara Administrator

Masomo ya siku hii Jumatano ya 24 ya Mwaka → 1Tim 3:14-16 · Zab 111: 1-6 · Lk 7:31-35
Kwenye somo la injili Yesu anakishangaa kizazi hiki kwani kinachezewa ngoma, kinaambiwa kifanye jambo hili lakini basi hakifuati. Kina ukaidi mkubwa na ukosefu wa upendo na hivyo basi kimeshindwa kutambua na kusoma alama za ulimwengu. Hii yote ni kwa sababu kilikosa upendo na kuwa na majivuno. Kikaona watu kama akina Yohane Mbatizaji na Yesu kama vituko tu. Kilitaka mawazo na mipango yao ifuate hali ya kuachana na wengine.

Sisi tuachane na mawazo kama haya ya hiki kizazi kwa kuwa watu wenye upendo zaidi, mshikamano na kuacha majivuno. Majivuno yametufanya tusiwe wa faida ndani ya ulimwengu.
0 Maoni
WhatsApp Facebook

Maoni (0)

Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.

Ingia utoe maoni