Ruka hadi maudhui
Mkatoliki Leo
Tafakari

Uvumilivu Utaokoa Maisha Yenu

· na Shajara Administrator

Masomo ya siku hii Jumatano ya 34 ya Mwaka → Ufu 15:1–4 · Zab 98:1–3, 7–9 · Lk 21:12-19
Tofauti na viongozi wengine ambao ni wabinafsi ambao wanapenda kujitafutia watu wengi na wafuasi wengi, Yesu mchungaji mwema na mkweli anasema wazi kabisa kuhusu dhoruba na adha zitakazo lipata Kanisa na mengi yatakayo wapata wafuasi wake. Kitabu cha ufunuo kiliandikwa ili kuwatia moyo wakristo walioteseka. Leo somo la kwanza, linapiga tarumbeta la wimbo wa ushindi wa waadilifu, waliojitoa na kuwa wafuasi waaminifu wa Mwana-kondoo. Katika familia zetu, katika sehemu zetu za kazi, katika parokia yetu, na sehemu nyingine nyingi tuna muda mzuri wa kushuhudia thamani ya Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Pengine mke msumbufu nyumbani, mume asiyejali, watoto wasumbufu na wasio tii, upweke katika maisha, maisha ya kukatisha tamaa, majirani tegemezi, kutokuelewana, uhusiano uliovunjika, magonjwa, ugumu wakupata fedha, ufisadi ulio kithiri, mumonyoko wa maadili,…hali zote hizi si mateso katika ufuasi wetu? “Huu ndio wakati wakutoa ushuhuda; kwa uvumilivu wenu, mtayaokoa maisha yenu” asema Bwana. Lakini ni nani kati yetu anayekubali kusimama pembeni na kuamua kuchagua njia wasio isafiri wengi, anayo isafiri Seremala wa nazareti?

Sala:
Bwana, tupe nguvu na roho yakuchagua njia yako na kukufuata wewe kwa uvumilivu.
Amina.
0 Maoni
WhatsApp Facebook

Maoni (0)

Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.

Ingia utoe maoni