Ruka hadi maudhui
Mkatoliki Leo
Tafakari

Upofu wa Kiroho

· na Shajara Administrator

Masomo ya siku hii Ijumaa ya 23 ya Mwaka → 1Kor 9:16–19, 22–27 · Zab 84:2–5, 7, 11 · Lk 6:39–42
Mfano kutoka katika Injili ya leo unatukumbusha ni kwa jinsi ghani ilivyo vigumu kwa kipofu kumuongoza kipofu mwenzake. Yesu haulizii kuhusu nguvu ya roho ya mwanadamu kushinda matatizo hayo. Anatuita tutambue upofu wa roho zetu. Tuombe ili upofu wa roho zetu wenyewe uweze kuponywa. Tunahitaji neema ili tuweze kuwa waaminifu kwa nafsi zetuni katika kutambua kikomo chetu, changamoto na udhaifu wetu.

Katika somo la kwanza Paulo anatuhimiza tupige mbio kila wakati tukililenga lile taji alilotuandalia Kristo mwenyewe kwani huo ndio ushindi wetu. Anatuhimizi tujifunze pia kuishi na wanyonge ili kwa hilo tuwapate wanyonge. Anatufundisha unyenyekevu katika maisha ya kumtangaza Kristo. Kwakufanya hivyo Injili tunayoihubiri italeta mafanikio kwa watu na zaidi sana kwetu sisi wenyewe. Paulo aliona pia hatari yakuweza kuwafundisha watu maneno ya Yesu na kuwasaidia lakini binafsi ukajisahau. Mhubiri wa kweli anajihubiria mwenyewe kwanza na baadae inatoka kwake na kuwagusa wengine. Kwahiyo Paulo anatuhimiza leo pia tuchunguze nafsi zetu kabla hatujaenda kwa wengine.

Sala:
Bwana, tusaidie tuweze kuwa Wafuasi wazuri. Tusaidie tuweze kujifunza jinsi ya kurekebisha maisha yetu wenyewe kabla hatuja angalia matendo ya wengine.
Amina
0 Maoni
WhatsApp Facebook

Maoni (0)

Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.

Ingia utoe maoni