Jumatano, Disemba 01, 2021
Jumatano , Desemba 1, 2021
Juma la 1 la majilio
Isa. 26:1-6;
Zab 118:1,8-9,19-21,25-27;
Mt 7:21.24-27
NI KITU GHANI KINATUFANYA TUSITIKISIKE?
Karibuni sana ndugu zangu wapendwa kwa adhimisho la misa takatifu asubuhi ya leo. Neno la Bwana katika Zaburi yetu ya wimbo wa katikati inazungumzia juu ya furaha na tamaa ya kutaka kukaa katika nyumba ya Bwana. Hakika kukaa kwenye nyua za Bwana, kuna faida zaidi kwani kukaa tu karibu yake litatuwezesha kukwepa madhambi mengi. Mara nyingi mazingira mabaya hutusababishia vishawishi, na wengi wetu tunaanguka dhambini baada ya kujiweka kwenye mazingira mabaya. Yafaa tupendelee kukaa kwenye mazingira yaliyo karibu na Bwana. Na kwa hakika tutashinda mengi.
Kipindi cha Majilio na kipindi cha kukaa karibu na Bwana.
Katika somo la injili, Makutano wamejitahidi kukaa na Bwana kwa muda mrefu. Na kwa kuwa wamekaa na Bwana, Bwana hawaachi waondoke pweke bali anawapatia chakula pia. Yesu hakutaka wakafie njiani, aliwapatia chakula bila ya wao kutegemea. Ndivyo ilivyo, ukikaa karibu na Bwana, Bwana atatujali.
Leo amewapatia makutano chakula. Hakika na sisi tusichoke kusali na kujiweka karibu na Bwana zaidi na zaidi.
Kwenye somo la kwanza, Nabii Isaya anatangaza ujumbe wa matumaini kwamba upo wakati ambapo aibu yetu na machozi yetu yatafutwa. Na Bwana atatuandalia karamu kuu kabisa, yenye utamu wa ajabu. Hakika kila mmoja wetu anaitamani siku hii.
Macho yetu na nyuso za wengi wetu zimejaa aibu. Tuna aibu ya magonjwa mbalimbali, tuna aibu ya umaskini na njaa na yote haya yanafanya nyuso zetu zijae aibu. Kwa hakika tunamhitaji Yesu afute aibu yetu. magonjwa yametupiga baadhi yetu hata tunakosa sura. Njaa imetudhoofisha baadhi yetu. Hakika tumejaa aibu sana kwa umaskini. Tumtegemee Yesu. Kwa hakika atafuta machozi yetu.
Maoni
Ingia utoe maoni