Ijumaa. 22 Novemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Januari 07, 2017

Jumamosi, Januari 7, 2017,

1 Yoh 5:14-21;
Zab 149: 1-6.9;
Yn 3:22-30.

KUBAKI DAIMA KWAKULITAZAMA FUMBO LA NOELI

Kwa wale ambao wameadhimisha Epifania siku ya ijumaa jana, Kesho, kipindi cha Noeli kinaisha kwa sikukuu ya ubatizo wa Bwana. Kuna hatari yakupoteza muelekeo wetu kwa Yesu, tukashindwa kuishi kama ilivyokuwa kipindi cha noeli kwasababu tu kipindi hiki kinaisha. Kama ilivyo, pengine wengi wetu tumesha haribu mipango yetu ambayo tulikuwa tumejiwekea mwaka huu mpya, kwasababu tumeanza kuifanya bila kumkabidhi Mungu, tukidhani tunaweza kuifanya wenyewe. Tukasahau nafasi ya Mungu.

Yohane Mbatizaji katika Injili anatambua nafasi ya Yesu. Yohane anatupa sisi msemo wa “Yeye aongezeke mimi nipungue”. Alijua kwamba yeye sio Masiha. Alitambua kuwa chochote kile alichofanya na kufanikiwa kilitakiwa kitoe sifa na njia kwa Masiha. Yohane alijutambua vizuri.

Changamoto kwetu sisi pia ni kujitambua. Tunapaswa kuacha kuyapa kipao mbele mambo yetu kwa nguvu zetu wenyewe na badala yake tujikabidhi mikononi mwa Mungu. Tunapaswa tutambue sisi ni wadogo na Mungu ni mkubwa wa yote. Tunapaswa tutambue kadiri tunavyo jinyenyekeza na kujishusha mbele ya Mungu, mapendo yetu kwake yanaongezeka.

Nyakati zetu ni rahisi kuwa wabinafsi sana kuliko hata kipindi chochote kile katika historia ya mwanadamu. Hii ni kwasababu wa ukuwaji wa sayansi na teknologia. Sisi daima tutambue nafasi ya mwanadamu mwenzangu daima ni muhimu na haiwezi kuondolewa na chombo chochote. Kwa upande mwingine tukiwa tumejikita na kujikabidhi kwa Yesu tusijisahau kutambue nafasi za wenzetu katika maisha yetu. Kama Yohane Mbatizaji, tunapaswa kuwa na utambuzi sahihi wa maisha yetu na ya wengine.
Tunapaswa kutambua vipaji vyetu, zawadi alizotupa Mungu, na wito wetu katika kutimiza mpango wa Mungu katika Maisha yetu. Pale ambapo hatuwezi tuwe tayari kujishusha kama Yohane tuwaachie wale wanaoweza, kwani kwa kufanya hivyo ni fadhila ya unyenyekevu.


SALA:Bwana Yesu, nivute karibu nawe zaidi, ili niweze kukuona wewe tuu. Ninaomba niishi maisha yangu, na katika uhusiano mzuri na wengine, katika kazi zangu bila kupoteza muelekeo wangu kwako daima. Yesu, nakuamini wewe. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni