Jumapili. 24 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Januari 17, 2021

Jumapili, Januari 17, 2021.
Juma la 2 la Mwaka wa Kanisa

Sam 3: 3-10; 19
Zab 39: 1-4-7,10
1Cor 6:13-15,17,20
Jh 1: 35-42


NZW, masomo yetu ya leo yanatualika kuiungama imani yetu ikiwa ni pamoja na kumtangaza YK ktk mazingira yetu. Sisi kama wafuasi wa YK, na kama wakristu tulio hai ni wajibu wetu kumtangaza YK kwa wengine. Kama sisi tunajinadi kuwa wakristo, tunashindwa je kumtangaza YK kwa wengine? Je ukristu wetu uko wapi? Masomo yetu ya leo yanatualika kuwajibika ktk hili.
Ktk somo la kwanza tumesikia jinsi Eli alivyomtambulisha kijana mdogo aitwaye Samueli kwa Mungu. Kijana huyu alikuwa hana maarifa au uelewa wowote juu ya mambo ya Mungu. Lakini Eli alimsaidia kuitika wito wa Mungu alipokuwa anaitwa. Na ni ktk njia hii Eli alimshirikisha Samueli ktk kumuelewa na kuyatambua mapenzi ya Mungu juu yake.
Ktk somo la pili, Mt. Paulo anawashirikisha wakorintho imani ya YK aliyoipata alipokuwa njiani kuelekea Damaskasi. Anawaambia kuwa wanapaswa kuishi kwa uaminifu ktk ukristu wao. Na ktk Injili, tunasikia jinsi Yohane Mbatizaji alivyowatambulisha wanafunzi wake wawili kwa YK ambaye ni Mtu kweli na Mungu kweli, kama “Mwanakondoo wa Mungu”. Na hao wanafunzi wanaamua kumfuata na kukaa pamoja naye. Mmojawapo wa hao wanafunzi alikuwa ni Andrea. Naye anachukua jukumu la kumleta Petro nduguye kwa BY na kumtambulisha kwake. Ktk injili ya nne ambayo ni ya Yohana, Andrea anaonekana kuwa na majukumu ya kuwatambulisha watu mbalimbali kwa BY. Katika Injili ya leo Andrea anamleta nduguye Petro kwa YK(Yh. 1/40). Pia kabla ya YK kuwalisha watu elfu tano kwa mikate mitano na samaki wawili, Andrea ndiye aliyemuonesha BY yule kijana aliyekuwa anauza hiyo mikate pamoja na hao samaki(Yh 6/8). Na kabla ya karamu ya mwisho, Andrea aliwatambulisha watu wa Kigiriki kwa BY(Yh 12/20-22). Hivyo Andrea anatambulika kwa kuwaleta watu kwa YK,ambaye ni Mtu kweli na Mungu kweli.


Sasa tujiulize maswali machache. Ni jinsi gani sisi tumejaribu kumtambulisha YK kwa wenzetu, au ni mara ngapi tumefanikiwa kuwaleta wenzetu kwa YK? Ni mambo gani yanayotufanya tushindwe kuikiri imani yetu mbele ya wenzetu? Vijana wa TYCS wana kauli mbiu yao ambayo ni kumleta YK ktk mazingira yao ikiwa ni pamoja na ktk familia wanazotoka. Je ni kweli wanatekeleza hili? Na kama tunaamini kwamba Injili ni habari njema sasa ni kwa nini tunashindwa kuwashirikisha watu wengine? Je tunaweza kujitetea kuwa sisi hatuna maarifa juu ya Mungu au hatumfahamu YK vizuri?
Wakati tunapokuwa na mambo mazuri yanayoifurahisha nafasi, huwa tunawashirikisha wenzetu. Kama ikitokea mtu akahujumiwa ktk mambo yale ayapendayo, utamsikia akisema “Aa, wameizulumu nafsi yangu bwana”. Lakini ni nini kilicho muhimu kwangu mimi zaidi ya imani yangu kwa BY? NZW tunapaswa kumtambulisha YK ktk mazingira yetu na kwa watu tunaoishi nao. Injili ya leo inatualika kuchukua hatua na kuacha ukaidi wetu wa kumtangaza YK kwa wengine. Kama tunaamini kwamba injili ni habari njema na, kuwa BY ni hazina kubwa inayomilikiwa na mioyo yetu, sasa ni kwa nini tunakuwa wagumu kuwashirikisha imani yetu tulionayo kwa watoto wetu, marafiki zetu na watu tunaoishi nao, na hasa wale ambao wanaitafuta imani hii? Hili ndilo swali muhimu ambalo lipo ktk injili yetu na kila mmoja wetu anapaswa kujiuliza. Hakuna mtu anayeweza kutusaidia kulijibu swali hili. Tunapaswa kulijibu sisi wenyewe kila mtu ktk muonekano wake. Ni dhahiri kwamba tunahitajika kuwajibika katika kumtangaza B.Y kwa watu wengine.

Basi tumwombe Mwenyezi Mungu atupe nguvu,uwezo na ujasiri ili tuweze kumtangaza B.Y ktk mazingira yetu na ktk jamii tunamoishi.

Maoni


Ingia utoe maoni