Jumapili. 24 Novemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Januari 02, 2021

Jumamosi, Januari 2, 2021,
Juma kabla ya Epifania

Kumbukumbu ya Watakatifu Basili Mkuu na Gregori Nazienzi

1 Yoh 2:22-28;
Zab 98: 1-4;
Yn 1:19-28.


UBATIZO, UHAI MPYA WA NEEMA.

Karibuni ndugu zangu katika adhimisho la misa Takatifu. Leo tunafanya kumbukumbu ya Watakatifu Basili na Greogori Nazianzeni, Maaskofu na Walimu wa Kanisa.

Tunachojifunza kikubwa katika Masomo yetu ni Ukuu alionao Kristo: Yesu aliyezaliwa duniani ni nafsi ya pili ya Utatu Mtakatifu. Yohane katika somo la kwanza anasema kwamba yeye (Yesu) ameunganika na Baba kwa undani wa pekee kiasi kwamba kila amkanaye Yesu, humkana na Baba pia. Huyo hatakuwa na mtetezi kwani Yesu ndiye hakimu na Baba amempa mamlaka juu ya vyote.

Yohane Mbatizaji katika injili ya leo haoni aibu kuushuhudia ukuu wa Yesu kwamba ni mkuu kuliko yeye kiasi kwamba hastahili hata kulegeza gidamu ya viatu vyake. Watakatifu Bazili Mkuu na Gregory Nazianze wanasifika kwa umahiri wao katika kuutetea Umungu wa huyu Yesu. Kwa pamoja waliupinga uzushi wa Ariani uliokataa ukuu na umoja wa Umungu wa Baba na wa Mwana. Watakatifu hawa wanaunganika na Yohane katika somo la kwanza kutuambia kwamba tukae ndani ya Kristo na tuyakatae mafundisho yote yanayompinga Kristo. Kazi tunazofanya zimtangaze Kristo; Tumshuhudie nyakati zote na mahali pote

Tumuombe Yesu tukisema, Ee Yesu uliyezaliwa duniani, nisaidie nisione aibu kukushuhudia wewe kwa maneno yangu, mawazo na matendo yangu.

Maoni


Ingia utoe maoni