Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Disemba 07, 2020

Desemba 7, 2020.

Jumatatu, JUMA LA 2 LA MAJILIO

Somo la 1: Isa 35:1-10 Isaya anatoa picha ya “nyakati za Masiha” ni katika uzuri wa jangwa linalo furahi na ubinadamu ulioponywa kutoka katika magonywa yote.

Wimbo wa katikati: Zab 85: 9-14 tazama, Mungu anakuja kutukomboa. Haki itamtangulia yeye….na Amani itafuata hatua zake.

Injili: Lk 5: 17-26 Sisi tunafanywa hai kiroho na kimwili kama yule aliyepooza. Yesu anathibitisha kwamba anauwezo wakusamehe dhambi kwa njia ya muujiza wa kuponya.

------------------------------------------------

TAMAA YA KUTAKA KUPONYWA NA KUSAMEHEWA

Katika somo la kwanza, nabii Isaya anatangaza ujio wa zama za Kimasiha ambao wale walio wanyonge, viwete, watafurahi, yaani maeneo yote yasio na matumaini, yatafurahi. Ujio wa Yesu ulizitimiza hizi zama. Nchi ilipata kufurahi na jangwa na palipo na ukiwa pakawa na furaha. Vilema waliruka ruka, bubu wakaongea, viziwi wakasikia, wenye njaa kupewa chakula na maskini kuhubiriwa habari njema. Hapa kwa kweli alitimiza zile zama za Kimasiha. Aliwaondolea watu vifungo vikubwa vya dhambi, vilivyoyafanya maisha yao na miili yao ipooze kama anavyomwondolea huyu mgonjwa anayemponya leo.

Hapa alimaanisha kwamba dhambi ni mbaya, haizoeleki, kwa sababu inafanya maisha ya mtu yapooze, yaparalyze, inaifanya jamii iparalyze. Hivyo isiachwe bila kukemewa. Kwa kufanya hivi, Yesu alituachia majukumu sisi wafuasi wake kwamba lazima tuendelee kuzitangaza zama hizi. Kutangaza zama za Kimasiha yamaanisha kwamba dhambi haivumiliwi, usione dhambi ushindwe kuikemea. Usione uovu unaendelea kutendeka wewe ukae kimya au ujiunge nao. Uovu huipoozesha roho, huparalyze maisha ya kiroho ya mkristo mwenyewe na jamii nzima. Na katika kitabu cha ufunuo, huu ujumbe unafanana na ule alioutoa Roho kwa kanisa ya Thiatira. Kanisa hili lilivumilia dhambi, lilishindwa kuwakemea wale wakristo MAARUFU, likavumilia dhambi zao na mwishowe wakaelekea kulibomoa kabisa. Roho aliliambia hili kanisa kwamba lisipotubu na kuwakemea hawa, litateketezwa na yule ambaye macho yake ni moto, akiangalia kitu-kiovu kinateketea chote. Hivyo, kama watu tunaotangaza zama za Kimasiha, tusiache hata siku moja kuikemea dhambi. Kemea uovu, uovu huteketeza jamii yote.

Penye kosa sema hapa pana kosa, usingate na kupuliza, hata kama ni maskini, hata kama ni mdogo mwambie umekosea, hata kama ni mtoto wako anayekupaga mchango mkubwa sana, akikosea mwambie hapa umekosea. Usipofanya hivyo jua unayapoozesha maisha yake na hata yako na baadaye ya jamii nzima.

Hata kama ni rafiki yako wa karibu-kama kakosea mwambie kakosea, mwambie hapa umechemka. Huu ndio ukristo. Hii kutafuta tafuta urafiki hapa, haiendi jamani, haiendi jamani. Tuombe nguvu kutoka kwa Yesu tuweze kutimiza hili kwa Imani kuu

Maoni


Ingia utoe maoni