Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Septemba 21, 2020

Jumatatu, Septemba 21, 2020,
Juma la 25 la Mwaka wa Kanisa

Sikukuu ya Mtakatifu Matayo Mtume na Mwinjili

Ef 4:1-7, 11-13
Zab 19:1-4
Mt 9: 9-13

MUNGU HAWAITI WAKAMILIFU, ANAWAPA UKAMILIFU WALE ALIO WAITA

Leo tuna sheherekea sikukuu ya Mtakatifu Matayo, mmoja wapo wa mitume kumi na mbili wa Bwana wetu Yesu Kristo. Alikuwa mtoza ushuru, alijulikana kama Lawi. Hapa anaitwa Matayo, maana yake “zawadi ya Mungu au aliyetolewa na Mungu”. Kama wale wakwanza wanne walio itwa na Yesu kwanza, Matayo, mtoza ushuru, aliacha kila kitu alichokuwa nacho na akamfuata Yesu. Wakati wa Yesu watu maarufu na watoza ushuru walikataliwa kama wadhambi kwa Wayahudi kadhalika na kwa Wayunani. Walikuwa na picha mbaya kiasa kwamba hata waombaji (omba omba) wenyewe walikataa kuomba chochote kutoka kwao. Ni katika utamaduni huu, Yesu alimuita Matayo/Lawi. Hii ni hali mpya ya kimapinduzi anayo fanya Yesu ili kujenga familia mpya ya Mungu.

Kuna vitu viwili tunaweza kujifunza kutoka kwa Matayo. Cha kwanza, alikubali mwenyewe wito wa Yesu. Wakati Mungu anapo ongea mmoja anaweza kupata kishawishi cha kusema ‘kesho; bado sijawa tayari’. Lakini Matayo mara moja aliitika wito wa Yesu. La pili, Matayo anaitwa akiwa katika mazingira ya hali yake ya maisha ya kawaida, wakati akijishughulisha na kazi yake. Yesu pia aliwaita mitume wa kwanza, Petro na Adrea, Yakobo na Yohane wakati wakiwa wakivua samaki. Leo tutambue kwamba sisi ni wadhambi lakini bado Mungu anatupenda, tumuombe nguvu zake na neema zake ili tuwe na maisha yenye kustahili wito wake.

Sala:
Bwana Yesu, tusaidie tuweze kuitika wito wako na tutangaze ujumbe wa Amani na upendo.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni