Kupoteza Maisha ya Nafsi Ili Kupata Yote
· na Shajara Administrator
Yesu anatuambia katika Injili kwamba, ni lazima kujikana nafsi ili kumfuata. Kujikana maana yake ni, kutokujibakiza, kutokujijengea heshima, kukataa, kujiachia, kujiweka huru kutoka mambo ya vionjo binafsi. Ni kusema “Ndio” kwa Kristo na kusema “Hapana” kwa nafsi. Sababu ya kujikana ni kwamba mioyo yetu ni muhimu zaidi kuliko ulimwengu mzima. Mwanadamu akishapoteza roho yake, imepotea haiwezi kununuliwa popote nakurudishwa. Mwanadamu atakaye ipoteza, ameipoteza milele. Msalaba unaonekana katika hali ya kawaida kama mateso na kupoteza, lakini kwa kweli ni faida. Sadaka ya Kristo Msalabani imekuwa fidia kubwa kwetu na kuleta wokovu. Je nipo tayari kujikana mwenyewe, kuchukua msalaba wangu na kumfuata Kristo?
Sala:
Mungu wangu, Mungu wangu, chukua yote kwangu yanayoniweka mbali nawe, Mungu wangu, Mungu wangu, nipe yote yanayo nileta karibu nawe, Mungu wangu, Mungu wangu, chukua ubinafsi ndani yangu na unipe yote katika wewe.
Amina.

Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni