Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Januari 25, 2020

Januari 25, 2020

JUMA LA 2 LA MWAKA WA KANISA

2Sam. 1:1-4, 11-12, 17, 19, 23-27
Zab. 80:1-2, 4-6 (K) 3
Mk 3: 20-21

VIPINGAMIZI KATIKA KUMFUATA YESU!

Yesu ni Hekima ya Mungu na ni Mungu. Kila kitu alichofanya na kusema kilifunua upendo kamili wa Utatu Mtakatifu. Baadhi ya watu walimsikiliza kwa makini na kwa Imani na utukufu wa mshangao kwa maneno yake na matendo yake. Waliweza kuona Umungu wake ukingaa na kutambua kweli alikuwa Mwana wa Mungu, mkombozi wa Ulimwengu. Lakini walikuwepo wengine, hata wengine waliokuwa ndugu zake, waliodhani “hayupo vizuri kiakili”.

Kama haya yalisemwa kwa Yesu pamoja na ukamilifu wake, yatasemwa pia kwetu tunaofuata njia zake. Kumfuata Yesu na kutimiza mapenzi yake sio kila mara itawapendeza ndugu zetu. Yapo mambo mengi tunayoitwa na Injili kufanya na kusema, ambayo yatapingwa tu na ndugu au jirani zetu. Wakati haya yanatokea, tusishangae au kuogopa au kutu umiza. Tusipatwe na hasira wala kukata tamaa. Bali, tunapaswa kujiona wenyewe tukifuata katika njia za Kristo. Tunapaswa kufikiria pia kuhusu kusingiziwa kwake kwa uongo na kuhukumiwa kwa uongo na tusikubali tunayosikia kwa wenzetu yatuweke mbali na kufuata mapenzi ya Mungu.

Sala:
Bwana, ninatambua kuwa ulishindwa kueleweka na ukahukumiwa vibaya na watu wengine, wengine watu wa wakaribu kabisa. Nisaidie daima niweze kukubali pale ninaposhindwa kueleweka katika maisha hasa pale ninapo kufuata wewe katika maisha. Nisaidie nikutafute wewe na kufanya mapenzi yako licha ya vipingamizi kutoka kwa wengine. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni