Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Januari 18, 2020

Januari 18 2020.

JUMAMOSI, JUMA LA 1 LA MWAKA

Somo la 1: 1 Sam 9:1-4,17-19, 10:1 somo linaelezea jinsi Saulo anavyochaguliwa Mfalme na kutawadhwa na Samweli.
Wimbo wa katikati : Zab 20:2-7 Ee Bwana, nguvu zako zinampa Mfalme furaha.

Somo la : Mk 2:13-17 Injili inaelezea wito wa Mathayo. Inaelezea pia hasira inayo wakumba Mafarisayo kwasababu ya kumuona Yesu akila chakula pamoja na watoza ushuru na wadhambi.


YESU NA HURUMA YAKE KWA WADHAMBI

Waisraeli sasa wana Mfalme, Saulo. Ni mtu aliye chaguliwa na Mungu mwenyewe, lakini pia ana uhuru wake wa kibinadamu, ni huru. Tutaona jinsi atakavyotumia uhuru wake vibaya na kupoteza kibali maChoni pa Mungu.

Katika Injili tunaona Yesu amemwita Mathayo (Lawi), mtoza ushuru, ambaye alikuwa anachukuliwa kama mtu aliye mbali na Ufalme wa Mungu, na anaitwa kuwa mwanafunzi wa Yesu. Lawi anaelewa thamani ya wito kutoka kwa Bwana na anataka kusherehekea na marafiki zake. Yeye anapanga sikukuu na amewaita marafiki zake, ili nao wapate kuitwa kufurahia ushirika wa kuwa na Yesu na wasitengwe mbali na huruma na msamaha wake.

Tunafurahi sana kuwanyoshea wengine vidole. Yesu pia alipingwa pia kwa kuwa karibu na wadhambi. Ukweli ni kwamba kila mmoja wetu isipokuwa Yesu, ni mdhambi. Yesu kwa uhuru kabisa muda mwingi alikuwa na wale ‘wasio tamanika’/wasio pendwa . hakuogopa kuonekana kuwa na hawa waliotengwa na jamii. Yesu pamoja na wafuasi wake waliwakaribisha watu hawa. Walikula na kunywa na watoza ushuru, makahaba, nk. Zaidi ya hayo waliwakaribisha hawa watu bila ya kuwahukumu au kuwaonyoshea kidole.

Je, upo tayari kujihusisha na wale wasio maarufu, wasio na kitu, walio umizwa, walio changanyikiwa, na wengineo? Je upo tayari kupoteza umaarufu wako kwasababu ya upendo na kujali kwa wale wasio na kitu? Upo tayari kufanya yote na kusaidia hata wale unaojua watakuharibia jina lako? Tunaitwa kushuhudia ujumbe huu wenye nguvu kutoka kwa Yesu. Tunaitwa kuwa na nguvu ya ujumbe huu wa Yesu unao watafuta daima walio potea na anaye muita kila mmoja wetu kufurahia urafiki naye. Kama Matayo na wafuasi wa Yesu tunaitwa kuwaita kwa Yesu wote waweze kupata ukaribu wa Yesu pamoja nasi.

Sala:
Bwana, unawapenda watu wote kwa mapendo ya ndani na upendo kamili. Ulikuja kwa ajili ya wale ambao maisha yao yalikuwa yamevunjika na wadhambi. Nisaidie niweze kuwatafuta wote walio wahitaji na kuwapenda wote kwa upendo usio na kipimo na kwa upendo usio wa kuhukumu. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni