Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Alhamisi, Disemba 12, 2019

Desemba 12, 2019.


ALHAMISI, JUMA LA 2 LA MAJILIO

Kumbukumbu ya Mt. Yahane wa Msalaba, Padre na Mwalimu wa Kanisa,

Somo la 1: Isa 41:13-20 Mungu anajiita mwenyewe kwamba “Ni Mtakatifu pekee wa Israeli na kuwahakikishia watu wakiwa katika mateso, anawaahidi upendo wake na kuwajalia na kutangaza utukufu wake na wao kuufurahia.

Wimbo wa Katikati: Zab 144:1, 9-13 Mungu ni mkarimu na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa mapendo. Yeye ni ufalme wa milele na utawala wake utatawala milele, kutoka karne hata karne.

Injili: Mt 11: 11-15 Yesu anamtambulisha Yohane Mbatizaji, anamuita mkuu kati ya wazawa wa wanawake, Elia ambaye alikuwa aje.

------------------------------------------------

JE, UNAHITAJI MSAADA WA MUNGU?

Kipindi cha majilio ni kipindi cha kutazamia na kutamani ujio wa Bwana, ni kipindi cha kutamani ujio wa Mungu hata Mungu mwenyewe anatamani sisi tuwe nae zaidi. Katika somo la Kwanza katika kitabu cha nabii Isaya, Mungu anahitaji kutambuliwa kwa yote ambayo amewatendea watu wake. Mungu anahimiza juu ya uhusiano: “mimi ni Bwana, Bwana Mungu wako, ambaye ninatambua mkono wako wa kuume ”. Mungu anatuita sisi kwa ujasiri wetu vilevile. Mara 11, Mungu ameonesha hilo “nitakusaidia”, nitakufanya kuwa mkuu…”nitakujibu..”nitajifunua….” “kwa Ukarimu,” “Mimi”, Mungu anaonesha kutaka kusaidia. “Ninataka kufanya mengi kwa ajili yako”.

Injili ya leo Yesu anaongelea kuhusu Yohane mbatizaji. Yohane alifungwa kwasababu ya kumkemea Herode, na hivyo akafungwa gerezani. Yesu anashuhudia utume wa Yohane na kumuongelea kama mtu mkuu. Lakini Yesu anadhihirisha kwa kusema kwamba walio wadogo katika ufalme wake ni mkuu zaidi kuliko Yohane. Aliye mdogo katika kumfuata Yesu na mwenye neema ya Yesu ni mkuu kuliko Yohane Mbatizaji, katika mambo ya kiroho na kushiriki kwake katika ufunuo wa yale yaliofunuliwa kwa mafumbo ya Ufalme wa Baba. Hili halina maana kwamba sisi ni watakatifu kuliko Yohane, au kwamba tunampendeza Mungu zaidi, au kwamba sisi ni muhimu zaidi katika historia au katika kanisa kuliko huyu Mtangulizi wa Kristo. Yesu alimaanisha kwamba sisi tunaufahamu mkubwa kuhusu ukombozi na kwamba tuna nafasi ya kushiriki kwa undani ndani ya Bwana kwani tumepokea ukamilifu wa Habari njema.

Je tunafanyaje hili? Je tunahitaji msaada wa Mungu, ukombozi wake tunauhitaji? Mungu anahitaji kufanya makuu kwa ajili yako. Kwa Yesu, Masiha, alikuja kutukomboa sisi. Je, tunapokeaje utajiri wake?

Sala:
Bwana, upo karibu. Wewe ni mkarimu na mwenye huruma, hukasiriki haraka mwingi wa huruma. Ninakuomba nifahamu unavyotamani mimi niwe nawe, ninakuomba niweze kuwa na shauku hiyo hiyo ya kutimiza mapenzi yako. Yesu nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni