Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Novemba 10, 2019

Jumapili, Novemba 10, 2019.
Juma la 32 la Mwaka C wa Kanisa

2 Mak 7:1-2, 9-14;
Zab 16: 1, 5-6, 8, 15;
2 The 2:16-3:5;
Lk 20:27-38.

MBINGUNI NI HAKIKA!

Katika Injili ya leo tunawaona Masadukayo wakijaribu kumtega Yesu kwa maswali kuhusu swala la ndoa na maisha baada ya kifo. Hili linafuata mtiririko wa Mafarisayo kutaka kumtega Yesu kwa kuleta swala juu ya kulipa kodi kwa Kaisari. Yesu anajibu hali zote katika hali ya urahisi kabisa.

Masadukayo walikuwa ni kikundi cha dini katika jumuiya ya Wayahudi. Walikuwa ni tofauti na Mafarisayo na walikubali vitabu vitano tu vya Biblia (Tora) na hawakukubali kuamini uwepo wa vitu kama Malaika, maisha baada ya kifo nk. Huku wakitaka kumtega Yesu walileta habari ya mwanamke na ndugu saba waliomuoa mwanamke huyo mmoja baada ya mwingine ili kutimiza sheria za Walawi za Kiyahudi kwamba mwanamume anapaswa kuoa mwanamke mmjane asiye na mtoto ili ampatie watoto ndugu yake aliyekufa bila mtoto. Swali ni kwamba, huyu mwanamke atakuwa wa nani katika maisha yajayo?

Jibu la Yesu lina sehemu mbili: kwanza, maelezo ya kufikirika kuhusu maisha yajayo na pili kuboresha jibu lake kutoka katika Tora (kwasababu Masadukayo waliamini Tora tu). Katika sehemu ya kwanza ya jibu la Yesu, anatofautisha sifa za maisha ya ulimwengu huu(duniani) na sifa za ulimwengu ujao (mbinguni) ili kurekebisha wanapokosea Masadukayo. Masadukayo katika kuongea kwao na kupinga ufufuko, wanachukua maisha ya mtu duniani na kuyafanya kuwa ni maisha ya mbinguni, walidhani kwamba kama kuna maisha baada ya kifo, basi kuoa na kuolewa kutaendelea huko pia. Jibu la Yesu lina sehemu mbili, “hawaoi wala hawaolewi kwasababu hawatakufa tena”-Yesu anataka kuwaambia kwamba kuoa na kuolewa inatakiwa hapa duaniani kwasababu wanadamu na uwepo wetu hapa ni wa muda tu. Kwahiyo, ndoa ni jambo jema ambalo mwanadamu anategemeza. Lakini katika maisha yajayo, hatufi tena kwahiyo Yesu anasema kwamba hakuna ndoa baada ya maisha haya. “Kwani watakuwa sawa na malaika”-baada ya kufa hatubebi tena miili yetu ambayo imeumbwa kuikabili dunia na tamaa zake bali tunakuwa na miili ya ufufuko, miili ya utukufu (kama ile ya malaika) na hivyo kuwa huru kuhusu mambo yote ya duniani au yote tulionayo hapa duniani . Kwahiyo hakuna ndoa katika maisha yajayo.

Katika sehemu ya pili, Yesu anatoa kithibitisho kutoka katika kitabu cha Kutoka, tunakopata habari ya Musa kukutana na Mungu katika kichaka kinacho waka moto. Yesu itakuwa aliamua kuchagua kutoa jibu lake kutoka katika kitabu hiki kusudi kabisa kwasababu Masadukayo wali amini tu Tora. Masadukayo waliamini kuhusu Mababu, kama Abrahamu, Isaka, Yakobo- ambao majina yao Musa aliyatamka katika mlima Sinai. Yesu anasema kuwa “kwakuwa Mungu sio wa waliokufa bali wanaoishi”, Abrahamu, Isaka na Yakobo lazima watakuwa wanaishi hata baada ya kufa kwao. Kwakutengeneza majibu ya namna hii kutoka katika maandiko, Yesu aliwanyamazisha Masadukayo, kama ilivyo andikwa katika kitabu cha Methali 26:27 –“kila achimbae shimo atatumbukia humo mwenyewe”. Masadukayo walichimba shimo ili kumtega Yesu lakini wao wenyewe wametumbukia humo.

Tuna ujumbe unaoendana katika somo la kwanza kutoka katika kitabu cha pili cha Makabayo tunaposikia kuhusu kifodini cha ndugu saba Wayahudi, ambao walikataa kuikana dini yao. Hawa 7 walitoa maisha yao wenyewe huku wakitangaza Imani yao juu ya ufufuko- mmoja wao alilia kwa sauti akisema “tutafufuliwa naye”. Mara nyingi tunaongea kuhusu maisha ya duniani kuwa mazuri kuishi lakini hapa tunaona Imani ya pekee kutoka kwa hawa ndugu saba wanao tufundisha kuhusu maisha ya umilele ambayo tutarithi tunastahili kufa kwa ajili ya hayo. Habari hii ya ndugu saba inatupa matumaini kwamba sisi nasi twaweza kuitangaza kama wao “tunakufa, ili tukaishi tena milele” . Ni hakika kwamba, kwa akili zetu zilizo na mipaka maisha baada ya kifo ni fumbo kubwa lisilo na jibu. Tunakuwa na mashaka na kuacha kuongea tunapo fikiri kuhusu ufufuko na maisha baada ya kifo, kwakuwa sisi ni wanadamu kama ilivyokuwa kwa wanafunzi baada ya kifo cha Yesu. Lakini walicho shikilia ni “tumaini’ na ni kitu ambacho sisi wote tunapaswa kushikilia. Kwahiyo tukiwa tumejazwa na Imani na matumaini tuamini alichotuambia Yesu –“ninaenda kuwaandalia makao”, kwasababu kila alichosema Yesu ni kweli tupu na alimanisha.

Tunapo elekea mwishoni mwa mwaka wa huruma ya Mungu tunapaswa kusisitiza ujumbe huu wa maisha baada ya maisha ya hapa duniani. Lakini kivipi? Tunatambua kuhusu matendo ya huruma aliotusisitizia Papa Fransisko kufanya, baadhi ya hayo ni kuwalisha wenye njaa, kuwavisha wasio na nguo, kuwatembelea wagonjwa na wafungwa, kuwasaidia maskini nk. Imani yetu kuhusu maisha yajayo inaimarishwa ndani mwetu na fadhila ya matumaini na kwakufanya matendo ya huruma kwasababu tunaenda kuwapa tumaini hili hili wengine waliolipoteza.

Sala:
Bwana Yesu, naomba niwe mjumbe wa matumani kwa ndugu zangu, na hasa kwa wale wanaoteseka.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni