Jumanne, Oktoba 01, 2019
Jumanne, Oktoba 1, 2019,
Juma la 26 la Mwaka
Zek 8: 20-23;
Zab 86: 1-7;
Lk 9: 51-56
KUKABILIANA NA KUKATALIWA!
Injili ya Luka leo, inanikumbusha kwamba, kwasababu tu watu hawaendani au hawakidhi viwango vyangu haimanishi tupaswa kuwahukumu. Mungu ametuumba sisi wote kama kiumbe pekee tulio na kazi ya kutimiza katika maisha. Pengine watu wa kijiji cha Samaria hawakuwa watu waliojali ujio wa Yesu, lakini kijiji kingine walichukua nafasi yao na kumjali. Hatupaswi kukata tamaa wakati maisha yanavyo “enda kinyume na mapenzi yetu”- bali tunapaswa kubaki katika uhusiano na Mungu kila mara, na kuamini kwamba kila tukio linatokea kwa lengo fulani. Tunapaswa kuwa watu wa sala na matumaini tusio na hofu na badala yake kuamini kwamba Mungu atatuongoza kwenye malengo yetu.
Yakobo na Yohane, walitaka mji wa Samaria ulaaniwe kwasababu haukumkaribisha Yesu, kwani walikuwa wameumizwa na kukataliwa. Kukataliwa na aina nyingine zinazo sababishwa na wengine zinaweza kuwa vigumu kuziachia ziondoke. Zinaweza kukaa ndani ya mioyo yetu na baadae kukuwa na kuchukuwa nafasi. Tukiwa na hali ya namna hii tutapata wakati mgumu sana wa kusamehe na kuachia mambo yatoke. Njia nzuri ya kuachia mambo yatoke ndani ya mioyo yetu ni kufanya kama Yesu alivyo fanya. Tunapaswa kuachia na kuendelea mbele. Mungu mwenyewe ndiye mwenye kulipiza sio kazi yetu. Tunavyo shindwa kufanya hili, maumivu yana tuumiza sisi zaidi kuliko mtu mwingine.
Tafakari leo juu ya kinyongo ulicho shikilia bado katika moyo wako kwasababu ya kuumizwa na mtu Fulani. Fanya uamuzi sahihi wa kusamehe na kusonga mbele. Kusamehe sio kujifanya kama vile kitendo ulicho tendewa hukufanyiwa wewe au basi tu. Bali, kitendo cha kumsamehe mwenzako ni hali ya kuonesha kuwa kulikuwa na kosa. Msamaha unakuruhusu wewe na kukupatia wewe nafasi ya kukuwa na kuachana na maumivu ambayo yangekupata kwasababu ya tendo ulilo fanyiwa. Lakini mwishoni linafungua mlango kwa aliyekosa kuweza kutubu na kutafuta msamaha nawe. Acha kisasi na lawama atoe Mungu na tafuta kuweka moyo wako katika Amani.
Sala:
Bwana, nina sali kwa ajili ya neema ya msamaha. Nina wasamehe wote walio niumiza mimi zaidi na nina wakabidhi kwako. Nawasamehe. Ninakupenda wewe Bwana wangu. Nisaidie mimi niwapende wengine kama wewe unavyo wapenda. Yesu, ninakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni