Ijumaa, Septemba 13, 2019
Ijumaa, Septemba 13, 2019.
Juma la 23 la Mwaka wa Kanisa
Kumbukumbu ya Mt. Yohane Krisostomi, Askofu na Mwalimu wa Kanisa
1 Tim 1:1-2, 12-14;
Zab 16:1-2,5,7-8, 11;
Lk 6: 39-42
Heshima na majitoleo
Tumeumbwa kushirikiana kama watu walio sawa na si kwa namna ya matabaka. Tunatakiwa kutambua vipawa vyetu na kushirikishana. Mt. Paulo anasema katika waraka wake wa kwanza kwa Timotheo kuwa, anakiri kuwa alitambua wito wake katika ujinga wake na katika kutokuamini kwake. Tuombe Neema hii aliyopokea Mt. Paulo ili nasi tubadilishwe katika maisha yetu.
Tunaalikwa kujifunza kutoka kwa wenzetu. Kila amtu anamtegemea mwenzake katika ufahamu na nguvu zinazotofautiana. Tunahitaji hekima na busara za majirani zetu. Papa Francis anasisitiza juu ya undugu katika kanisa zima kwa ujumla.
Mambo tusiyoweza kuona
Kwasababu hatujakamilika katika kung’amua mambo ya watu wanaotuzunguka, inakuwa rahisi sana kuhukumu wengine. Tunaweza kusema kuwa sote tunaweza kuona lakini kiuhalisia baadhi yetu ni vipofu. Bwana wetu Yesu Kristo anatuonesha kuwa sisi ni vipofu kwa namna Fulani, na mara nyingi kipofu anamuongoza kipofu. Mara chache sana mtu aonaye kumuongoza yule aliye kipofu.
Yesu anatubadilishia mfano ili tuweze kumuelewa Zaidi. Yesu anatupa mfano wa mtu anayetazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yake, na boriti iliyo ndani yake mwenyewe haiangalii.Yesu anaposema kutoa boriti kwanzaa kwenye jicho lako mwenyewe maana yake kutambua madhaifu yetu kabla ya kuona madhaifu ya wengine. Mara nyingi tunashindwa kutambua kinachoendelea katika maisha ya wenzetu hivyo tunaishia kuwahukumu tu. Mungu anayeona undani kila moyo, ni mwenye huruma kwa wote hata kwa wale wasiostahili. Leo tunaalikwa kuwa na huruma na msamaha kwa wengine.
Maoni
Ingia utoe maoni