Jumamosi, Agosti 17, 2019
Jumamosi, Agosti 17 2019
Juma la 19 la Mwaka
Kumbukumbu ya Bikira Maria
Yos 24: 14-29;
Zab 15: 1-2, 5, 7-8, 11;
Mt 19:13-15
KUMPOKEA YESU KAMA WATOTO!
Leo somo la Injili kwa ufupi linaelezea jinsi Yesu alivyo wakubali watoto. Wafuasi wanawazuia watoto, pengine ni kwasababu ya sheria ya kujiweka safi. Watoto wadogo katika hali walizokuwa wakiishi ilikuwa inachukuliwa kuwa sio safi, rahisi kuchafuka. Kama walitaka kumgusa Yesu wangemchafua pengine. Yesu hajali kuhusu sheria ya usafi isiyojali undugu na kumrusu kuwa na wadogo. Upya katika Mungu, Baba aliye ndani ya Yesu anayaweka alama maisha ya Yesu na anampa macho mapya ya jinsi ya kutufundisha kuthamini na kujali uhusiano kati ya watu. Yesu anakuwa upande wa watoto waliotengwa na anakuwa mlinzi na kinga kwao.
Inavutia sana kuhusu Biblia na hasa tabia ya Yesu kuwajali watoto na kuwalinda, watoto wanaelewa kuhusu mambo ya Ufalme aliotangaza vizuri zaidi kuliko wale waliojiona waelewa. (Mt 11:25-26). Wanapokea bila kubadili maana na kukwaza. Kati ya maneno makali ya Yesu ni kuhusu wanaosababisha makwazo kwa walio wadogo, akimaanisha wale wanaosababisha wadogo wasiwe na Imani kwa Mungu. Kwasababu ya hili, ni bora wangefungwa jiwe la kusagia shingoni na kutupwa baharini (Lk 17:1-2; Mt 18:5-7). Yesu anawataka wafuasi wawe kama watoto wadogo ili waweze kuupokea Ufalme kama watoto wanavyopokea. Bila kuwa hivi, itakuwa vigumu kuingia kataka Ufalme wa Mungu (Lk 9:46-48). Ina maana kwamba watoto wamefanywa kuwa walimu wa wakubwa. Watoto ni wanyofu daima, wanawategemea wazazi bila kuwa na wasiwasi, sisi nasi tumtegemee Mungu bila kuwa na wasi wasi tukiwa na mioyo minyofu kama watoto.
Tafakari leo juu ya jinsi Yesu anavyo kugusa ndani unavyo mpokea katika komunyo Takatifu. Je, upo tayari kwa yale yote ambayo anapenda kuyaweka ndani mwako? Tazama upya juu ya uwazi wa roho yako kwake na tafuta jinsi ya kumkaribisha ndani ya roho yako kwa undani zaidi unapo simama kwenda kumpokea.
Sala:
Bwana, ninakupenda wewe na ninatamani kufungua moyo wangu zaidi katika kukupokea katika komunyo Takatifu. Ninaomba nifungue moyo wangu kwa kila kitu ambacho unatamani kuweka ndani ya moyo wangu. Njoo moyoni mwangu Bwana Yesu, na badilisha maisha yangu kwa kunigusa mimi. Yesu nakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni