Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Agosti 03, 2019

Jumamosi, Agosti 3, 2019
Juma la 17 la Mwaka wa Kanisa

Wal. 25:1,8-17
Zab 67:2-3,5-8
Mt. 14:1-12

CHUKI NA KISASI

Katika somo la Injili la leo tunasikia kuhusu kukatwa kichwa kwa Yohane Mbatizaji kwasababu ya ombi la Salome, binti wa Herodia. Yohane alikuwa gerezani kwasababu ya kuongea ukweli kuhusu Herodi kumchukua mke wa nduguye, na hivyo Yohane alichukiwa na Herodia. Hivyo mtoto wa Herodia alivyo cheza vizuri mbele ya Herodi Mfalme na wageni wake, Herodi alipendezwa sana na kucheza kwa binti huyu na hivyo kumwambia aombe lolote kwake naye binti anaomba kichwa cha Yohane mbatizaji baada ya kuomba ushauri kwa mama yake. Hivyo kwanini Herodia na mtoto wake wanaomba kichwa cha Yohane Mbatizaji?

Herodi alikuwa mtu wa kidunia. Pengine Herodia alikuwa na vinywaji vingi sana siku hiyo katika siku hii yake ya kuzaliwa; na katika furaha hii anafanya uamuzi ambao sio wa hekima, ambao Herodia anatumia muda huu kutimiza maovu yake. Herodi anafanya uamuzi ambao yeye mwenyewe hakutaka hivyo anaogopa kutenda mema. Anajazwa na chuki ya mke wake huyu na hivyo, anaamua Yohane akatwe kichwa yeye ambaye alikuwa amemzoea kumsikiliza na kufurahi. Herodia hakuwa na dhamiri hai yenye kumkataza kufanya uovu. Aina hii ya chuki inaeleza jinsi ghani chuki ilivyo mbaya inavyokuwa kubwa huleta madhara. Wakati hasira inavyokuwa huleta madhara makubwa mno na kusababisha uharabifu mkuwa sana katika maisha yetu na ya watu. Hali hii ya hasira inapaswa kufanyiwa toba na kusamehewa mwanzoni kabisa kabla haijawa kubwa.

Tafakari leo, je, umeshikilia hasira ambayo ni mbaya na kinyongo moyoni mwako katika hali yeyote? Je, hasira hiyo inakuwa nakusababisha hasara kwako na kwa wengine? Kama ndiyo hivyo, jitahidi kuiacha na samehe na anza maisha mapya. Ndilo jambo jema ambalo waweza kulifanya.

Sala:
Bwana, ni pe neema ninayo hitaji ili niweze kutazama moyo wangu au uchungu wowote ndani yangu au chuki yeyote ile. Nisafishe Bwana na nakuomba unifanye niwe huru. Yesu, nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni