Jumatatu. 29 Aprili. 2024

Sala

Sala ya Asubuhi

Siku mpya inaanza ,
nimwabudu Mungu kwanza
Mungu wangu baba yangu,
upokee shukrani zangu
Wewe kwa usiku mzima,
ulikuwa kwangu daima
Kunilinda kwa amani,
na mitego ya shetani
Kwako baba wa milele,
ninaomba neema tele
Niepuke dhambi zote,
nikutumikie kote
Ubariki kazi yangu,
shida na furaha zangu
Mama safi eeh Maria,
nipe msaada wako pia
Malaika kiongozi,
nipeleke kwa mwokozi
Yesu nijalie neema
niwe daima mkristo mwema

Amina

Maoni


Ingia utoe maoni