Alhamisi ya Oktava ya Pasaka
· Mwaka B · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mdo 3:11-26Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 8:1, 4-8Wewe, Mungu, Bwana wetu
Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni;
Mtu ni kitu gani hata umkumbuke,
Na binadamu hata umwangalie?
(K)Ee, Mungu, Bwana wetu; jinsi lilivyo tukufu jna lako duniani mwote.
Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu;
Umemvika taji ya utukufu na heshima;
Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;
Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
(K)Ee, Mungu, Bwana wetu; jinsi lilivyo tukufu jna lako duniani mwote.
Kondoo, na ng'ombe wote pia;
Naam, na wanyama wa kondeni;
Ndege wa angani, na samaki wa baharini;
Na kila kipitacho njia za baharini.
(K)Ee, Mungu, Bwana wetu; jinsi lilivyo tukufu jna lako duniani mwote.
Injili
Lk 24:35-48Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko. Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni