Sikukuu ya Watakatifu Simoni na Yuda, Mitume
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Efe. 2:19-22Tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kuku ahata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 19:1-4Sauti yao imeenea duniani mwote.
Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu,
Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.
Mchana husemezana na mchana,
Usiku hutolea usiku maarifa.
K. Sauti yao imeenea duniani mwote.
Hakuna lugha wala maneno,
Sauti yao haisikilikani.
Sauti yao imeenea duniani mwote,
Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.
Katika hizo ameliwekea jua hema.
K. Sauti yao imeenea duniani mwote.
Shangilio la Injili
ShangilioInjili
Lk. 6:12-16Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni