SIKUKUU YA WATAKATIFU MIKAELI, GABRIELI NA RAFAELI
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Dan. 7:9-10,13-14Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 138:1-5Nitakushukuru kwa moyo wangu wote,
Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu. (K) Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako,Kwa maana umeikuza ahadi yako,Kuliko jina lako lote.Siku ile niliyokuita uliniitikia,Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu. (K) Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
Ee Bwana, wafalme wote wa dunia watakushukuru,Watakapoyasikia maneno ya kinywa chako.Naam, wataziimba njia za Bwana,Kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu (K) Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
Shangilio la Injili
Zab. 105:3Aleluya, aleluya,
Mhimidini Bwana, enyi majeshi yake yote, ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake.
Aleluya.
Injili
Yn. 1:47-51Yesu alipomwona Nathanaeli anakuja kwake akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake. Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwa chini ya mtini nilikuona. Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli. Yesu akajibu, akamwambia, kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya. Akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni