Jumamosi katika Oktava ya Pasaka
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mdo. 4:13 – 21Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 118:1, 14 – 21Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Aleluya,
Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema,
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu,
Naye amekuwa wokovu wangu.
Sauti ya furaha na wokovu,
Imo hemani mwao wenye haki.
K. Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Au Aleluya
Mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu.
Mkono wa kuume wa Bwana umetukuzwa;
Mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu.
Sitakufa bali nitaishi,
Nami nitayasimulia matendo ya Bwana.
Bwana ameniadhibu sana,
Lakini hakuniacha nife.
K. Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Au Aleluya
Nifungulieni malango ya haki,
Nitaingia na kumshukuru Bwana.
Lango hili ni la Bwana,
Wenye haki ndio watakaoliingia.
Nitakushukuru kwa maana umenijibu,
Nawe umekuwa wokovu wangu.
K. Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Au Aleluya
Shangilio la Injili
Zab. 118:24Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana, Tutaishangilia na kuifurahia.
Aleluya.
Injili
Mk. 16:9 – 15Baada ya hayo akawatokea watu wawili miongoni mwao, ana sura nyingine; nao walikuwa wakishika njia kwenda shamba. Na hao wakaenda zao wakawapa habari wale wengine; wala hao hawakuwasadiki.
Baadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu. Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni