Ijumaa ya 20 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Eze 37:1-14Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 107:2-9Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni Mwema. Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Na waseme hivi waliokombolewa na Bwana, Wale aliowakomboa na mkono wa mtesi.
Akawakusanya kutoka nchi zote, Mashariki na magharibi, kaskazini na kusini.
K. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni Mwema. Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Walitanga-tanga jangwani katika njia ya nyika; Hawakuona mji wa kukaa.
Waliona njaa, waliona na kiu, Nafsi yao ilikuwa ikizimia ndani yao.
K. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni Mwema. Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao.
Akawaongoza kwa njia ya kunyoka, Wapate kwenda mpaka mji wa kukaa.
K. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni Mwema. Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Na wamshukuru Bwana, kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.
Maana hushibisha nafsi yenye shauku, Na nafsi yenye njaa huijaza mema.
K. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni Mwema. Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Shangilio la Injili
Zab 117:7,8Maagizo yako yote, ee Bwana ni amini, yamethibitika milele na milele
Aleluya
Injili
Mt 22:34-40Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
Arbogast Munishi · 21 Agosti 2026
Naomba uruhusu tuweze kuona somo linalofuata ili mtu aweze kufanya maandalizi. Asante