Jumanne ya 17 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yer 14:17-22Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 79:8-9,11, 13Kwa ajili ya utukufu wa jina lako, utusaidie, Ee Bwana.
Usikumbuke juu yetu maovu ya baba zetu,
Rehema zako zije kutulaki hima.
Kwa maana tumedhilika sana.
K. Kwa ajili ya utukufu wa jina lako, utusaidie, Ee Bwana.
Ee Mungu wa wokovu wetu, utusaidie,
Kwa ajili ya utukufu wa jina lako.
Utuokoe, utudhofiri dhambi zetu,
Kwa ajili ya jina lako.
K. Kwa ajili ya utukufu wa jina lako, utusaidie, Ee Bwana.
Kuugua kwake aliyefungwa na kuingia mbele zako,
Kwa kadiri ya uwezo wa mkono wako
Uwahifadhi wana wa mauti.
Na sisi tulio watu wako, na kondoo za malisho yako,
Tutakushukuru milele;
Tutazisimulia sifa zako kizazi kwa kizazi.
K. Kwa ajili ya utukufu wa jina lako, utusaidie, Ee Bwana.
Shangilio la Injili
Ebr 4:12Neno la Mungu li hai tena li na nguvu, li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Aleluya.
Injili
Mt 13:36–43Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
Sebastian Mavukilo · 28 Julai 2026
Eeh Baba Mungu tunakuomba utujalie mioyo ya utii na unyenyekevu juu yako; juu ya Neno lako, AMRI zako na SHERIA zako. Siku zote tuutafute uso wako kwa BIDII na uvumilivu mkubwa. Tunakuomba Eeh Mungu usizitazambe dhambi zetu bali IMANI ya kanisa lako, ututenge na hukumu ya dhambi zetu za zamqni na dhambi za wazee wetu. Usutukasirikie Mungu wetu ili adui asijiinue kwa sababu ya shida zetu. Wewe ndio Mungu muweza wa yote, ngome na kimbilio letu. Ni katika jina la YESU KRISTO Bwana wetu tunaomba na kushukuru. Amina.