Kumbukuku ya Mtakatifu Martha
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yer 15:10, 16-21Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 59:2-4, 10-11, 17-18Bwana alikuwa ngome yangu siku ya shida yangu
Ee Mungu wangu, uniponye na adui zangu, Uniinue juu yao wanaoshindana nami.
Uniponye nao wafanyao maovu, Uniokoe na watu wa damu.
K. Bwana alikuwa ngome yangu siku ya shida yangu
Kwa maana wanaiotea nafsi yangu; Wenye nguvu wamenikusanyikia;
Ee Bwana, si kwa kosa langu, Wala si kwa hatia yangu.
K. Bwana alikuwa ngome yangu siku ya shida yangu
Ee nguvu zangu, nitakungoja Wewe, Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu
Mungu wa fadhili zangu atanitangulia, Mungu atanijalia kuwatazama adui zangu.
K. Bwana alikuwa ngome yangu siku ya shida yangu
Nami nitaziimba nguvu zako asubuhi, Nitaziimba fadhili zako kwa furaha.
Kwa kuwa ndiwe uliyekuwa ngome yangu, Na makimbilio siku ya shida yangu.
K. Bwana alikuwa ngome yangu siku ya shida yangu
Ee nguvu zangu, nitakuimbia kwa furaha,
Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu, Mungu wa fadhili zangu.
K. Bwana alikuwa ngome yangu siku ya shida yangu
Shangilio la Injili
Yak 1:21Pokeeni kwa upole neno la Mungu lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.
Aleluya.
Injili
Yn 11:19-27Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni