Alhamisi ya 16 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yer 2:1–3, 7–8, 12–13Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 36:5–10Kwako Bwana iko chemchemi ya uzima.
Ee Bwana, fadhili zako zafika hata mbinguni,
Uaminifu wako hata mawinguni.
Haki yako ni kama milimo ya Mungu,
Hukumu zako ni vilindi vikuu.
K. Kwako Bwana iko chemchemi ya uzima.
Ee Bwana, unawaokoa wanadamu na wanyama.
Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhila zako!
Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako.
Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako,
Nawe utawanywesha mto wa furaha zako.
K. Kwako Bwana iko chemchemi ya uzima.
Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima,
Katika nuru yako tutaona nuru.
Uwadumishie wakujuao fadhili zako,
Na wanyofu wa moyo uaminifu wako.
K. Kwako Bwana iko chemchemi ya uzima.
Shangilio la Injili
Zab 147:12, 15Msifu Bwana, ee Yerusalemu, huipeleka amri yake juu ya nchi.
Aleluya.
Injili
Mt 13:10–17Lakini, heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia. Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
Sebastian Mavukilo · 23 Julai 2026
Tumsifu Yesu Kristo wapendwa, Leo tunaona Mungu anavyotukumbusha kipindi tulipokuwa watii na neema na ulinzi ambao anatupatia katika hali hiyo. Pia, anaonyesha masikitiko makubwa kutokana na uhasi na mioyo migumu yetu ambayo hupelekea mambo mengi mema aliyotupanhia kuhalibika, tunayanajisi sisi wenyewe. Mioyo hii migumu alikutana nayo pia Bwana wetu Yesu Kristo, aliye chemchemi na asili ya uzima wetu, na kweli yote. Lakini licha ya watu kumuona na kuzungumza nae, bado hawakutaka kusadiki. Hali ilimlazimisha kutumia mifano ili angalau kuwarahisishia watu kuelewa au kutoa hofu kidogo. Hivyo, na sisi leo, tumwombe Mungu atujalie nguvu za Roho wake Mtakatifu ili tuwe na mioyo myepesi, yenye kupokea na kuliishi NENO la Mungu.