Dominika ya 16 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Hek 12 :13.16-19Pamoja na hayo, uliwafundisha watu wako kwa matendo yako ya namna hiyo ya kwamba imempasa mwenye haki kuwa mpenda wanadamu; tena ukawatilia wanao tumaini jema, kwa sababu, endapo watu wametenda dhambi, unawajalia toba.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 86:5-6, 9-10, 15-16Kwa maana Wewe, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe.
Wewe, Bwana, U mwema,
Umekuwa tayari kusamehe.
Na mwingi wa fadhili,
Kwa watu wote wakuitao.
Ee Bwana, uyasikie maombi yangu;
Uisikilize sauti ya dua zangu.
K. Kwa maana Wewe, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe.
Mataifa yote uliowafanya watakuja;
Watakusujudia Wewe, Bwana.
Watalitukuza jina lako;
Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu.
Wewe ndiwe mfanya miujiza,
Ndiwe Mungu peke yako.
K. Kwa maana Wewe, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe.
Lakini Wewe, Bwana,
U Mungu wa rehema na neema.
Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli.
Unielekee na kunifadhili mimi.
K. Kwa maana Wewe, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe.
Somo la Pili
Rum 8:26-27Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Yn 17:17Neno lako ndiyo kweli,
Ee Bwana, Ututakase sisi kwa ile kweli.
Aleluya.
Injili
Mt 13:24-43Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (6)
Linus Bernard · 19 Julai 2026
MWENYEZI MUNGU awabaliki sana kwa kunipatie njia rahisi na wepesi wa kusoma neno la Mungu,hata nisipofika kanisa lakini nimekuwa nikifatilia masomo yote kupitia Mkatolikileo.
Sebastian Mavukilo · 19 Julai 2026
Mungu awabariki sana kwa uinjilisti huu. Tumuombe mwenyezi Mungu atujalie nguvu za Roho Mtakatifu ili tusijikute tumekuwa sehemu ya magugu. Tujitahidi kuikimbia dhambi kwa kumkataa shetani na njia zake zote. Muwe na Dominika njema watu wa Mungu
Kamgisha Elipidius · 19 Julai 2026
Asante kaka hakika tutaikimbia dhambi
Kamgisha Elipidius · 19 Julai 2026
Nalifurahia neno la mungu mfalme wa amani bwana mungu nitetee na watesi wangu wasinifikie
MARCO Cletus · 19 Julai 2026
Yaan zaburi ya leo imenyooka Ni vile uwe mwema bac uwe tayar kusamehe
Egrasius Salvatory · 19 Julai 2026
Mungu tusamehe dhambi zetu
Egrasius Salvatory · 19 Julai 2026
Tujalie amani ya kristo