Jumamosi ya 11 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
2Nya 24:17–25Na roho ya Mungu ikamjia Zekaria, mwana wa Yehoyada, kuhani; naye akasimama juu ya watu, akawaambia, Mungu asema hivi, Kwani ninyi kuzihalifu amri za Bwana, hata msiweze kufanikiwa? Kwa kuwa mmemwacha Bwana, yeye naye amewaacha ninyi. Basi, wakafanya shauri juu yake, wakampiga kwa mawe kwa amri ya mfalme, katika ua wa nyumba ya Bwana. Basi hivyo mfalme Yoashi hakuukumbuka wema, ambao Yehoyada, baba yake, alimfanyia, bali alimwua mwanawe. Naye alipokufa, alisema, Bwana na ayaangalie haya, akayatakie kisasi.
Ikawa mwisho wa mwaka, wakakwea juu yake jeshi la Washami; wakafika Yuda na Yerusalemu, wakawaangamiza wakuu wa watu wote miongoni mwa watu, wakamletea mfalme wa Dameski nyara zao zote. Maana wakaja jeshi la Washami watu haba; Bwana akatia mikononi mwao jeshi kubwa mno, kwa sababu wamemwacha Bwana, Mungu wa baba zao.
Hivyo wakamfanyia Yoashi hukumu. Hata walipoondoka kwake, (nao walimwacha ameshikwa sana na maradhi) watumishi wake mwenyewe wakamfanyia fitina kwa ajili ya damu ya mwana wa Yehoyada kuhani, wakamwua kitandani pake, akafa; wakamzika mjini mwa Daudi, lakini hawakumzika katika makaburi ya wafalme.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 89: 3-4, 28–33Nitamwekea fadhili zangu milele.
Nimefanya agano na mteule wangu,
Nimemwapa Daudi, mtumishi wangu.
Wazao wako nitawafanya imara milele,
Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele.
K. Nitamwekea fadhili zangu milele.
Hata milele nitamwekea fadhili zangu,
Na agano langu litafanyika amini kwake.
Wazao wake nao nitawadumisha milele,
Na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu.
K. Nitamwekea fadhili zangu milele.
Wanawe wakiiacha sheria yangu,
Wasiende katika hukumu zangu,
Wakizihalifu amri zangu,
Wasiyashike maagizo yangu.
K. Nitamwekea fadhili zangu milele.
Basi, nitawarudi makosa yao kwa fimbo,
Na uovu wao kwa mapigo.
Lakini fadhili zangu sitamwondolea yeye,
Wala sitafanya uaminifu wangu kuwa uongo.
K. Nitamwekea fadhili zangu milele.
Shangilio la Injili
Zab. 119: 135Umwangazie mtumishi wako uso wako, na kunifundisha amri zako.
Aleluya.
Injili
Mt 6:24–34Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni