Ijumaa ya 26 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Bar 1:15-22Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 79:1-6, 8-9Utusaidie, Ee Mungu, kwa ajili ya utukufu wa jina lako.
Ee Mungu, mataifa wameingia katika urithi wako,
Wamelinajisi hekalu lako takatifu.
Wamefanya Yerusalemu chungu chungu.
Wameziacha maiti za watumishi wako
Ziwe chakula cha ndege wa angani.
Na miili ya watauwa wako Iwe chakula cha wanyama wa nchi.
K. Utusaidie, Ee Mungu, kwa ajili ya utukufu wa jina lako.
Wamemwaga damu yao kama maji
Pande zote za Yerusalemu,
Wala hapakuwa na mzishi.
Tumekuwa lawama kwa jirani zetu,
Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.
Ee Bwana, hata lini? Utaona hasira milele?
Wivu wako utawaka kama moto?
K. Utusaidie, Ee Mungu, kwa ajili ya utukufu wa jina lako.
Usikumbuke juu yetu maovu ya baba zetu,
Rehema zako zije kutulaki hima.
Kwa maana tumedhilika sana.
K. Utusaidie, Ee Mungu, kwa ajili ya utukufu wa jina lako.
Ee Mungu wa wokovu wetu, utusaidie,
Kwa ajili ya utukufu wa jina lako.
Utuokoe, utughofiri dhambi zetu,
Kwa ajili ya jina lako.
K. Utusaidie, Ee Mungu, kwa ajili ya utukufu wa jina lako.
Shangilio la Injili
Yn 10:27Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata.
Aleluya.
Injili
Lk 10:13–16Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni