Alhamisi ya 19 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yos 3: 7-11, 13-17Basi Yoshua akawaambia wanu Israeli, Njoni huku, mkayasikie maneno ya Bwana, Mungu wenu. Yoshua akasema, kwa jambo hili mtajua ya kuwa Mungu aliye hai yu kati yenu, na ya kuwa hatakosa kuwatoa mbele yenu Mkanaani, na Mhiti, na Mhivi, na Mperizi, na Mgirgashi, na Mwamori, na Myebusi. Tazama, sanduku la agano la Bwana wa dunia yote linavuka mbele yenu na kuingia Yordani. Itakuwa, wakati nyayo za makuhani walichukao sanduku la Bwana, Bwana wa dunia yote, zitakaposimama katika maji ya Yordani, hayo maji ya Yordani yatatindika, maji yale yashukayo kutoka juu; nayo yatasimama kama chuguu.
Hata ikawa, hao watu walipotoka katika hema zao, ili kuvuka Yordani, makuhani waliolichukua sanduku la agano wakatangulia mbele ya watu, basi hao waliolichukua hilo sanduku walipofika Yordani, na nyayo za makuhani waliolichukua sanduku zilipotiwa katika maji ya ukingoni, (maana Yordani hujaa hata kingo zake na kufurika wakati wote wa mavuno,) ndipo hayo maji yaiiyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa chuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyotelemkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yakatindika kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko. Na hao makuhani waliolichukua sanduku la agano la Bwana wakasikamama imara mahali pakavu katikati ya Yordani; Israeli wote wakavuka katika nchi kavu, hata taifa lile lote likaisha kuvuka Yordani.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 114 :1-6Aleluya.
Aleluya.
Israeli alipotoka Misri,
Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni.
Yuda ilikuwa patakatifu pake,
Israeli milki yake.
K. Aleluya.
Bahari iliona ikakimbia,
Yordani ilirudishwa nyuma.
Milima iliruka kama kondoo waume.
Vilima kama wana-kondoo.
K. Aleluya.
Ee bahari, una nini, ukimbie?
Yordani, urudi nyuma?
Enyi milima, mruke kama kondoo waume?
Enyi vilima, kama wana-kondoo?
K. Aleluya.
Shangilio la Injili
Efe 1: 17, 18Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristu,
awape roho ya hekima mjue tumaini la mwito wake.
Aleluya.
Injili
Mt 18:21 - 19:1Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni