Sikukuu ya Kung’ara Bwana Wetu
· Mwaka B
Somo la Kwanza
Dan 7: 9-10, 13-14Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu nave. Nave akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo haitapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 97: 1-2, 5-6, 9Bwana ametamalaki, juu sana kuliko nchi yote.
Bwana ametamalaki, nchi na ishangilie,
Visiwa vingi na vifurahi.
Mawingu na giza vyamzunguka,
Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake.
K. Bwana ametamalaki, juu sana kuliko nchi yote.
Milima iliyeyuka kama nta mbele za Bwana,
Mbele za Bwana wa dunia yote.
Mbingu zimetangaza haki yake,
Na watu wote wameuona utukufu wake.
K. Bwana ametamalaki, juu sana kuliko nchi yote.
Maana Wewe, Bwana, ndiwe Uliye juu,
Juu sana kuliko nchi yote;
Umetukuka sana juu ya miungu yote.
K. Bwana ametamalaki, juu sana kuliko nchi yote.
Somo la Pili
2Pet 1:16-19Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Mt 17: 5Huyu ni mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye, msikieni yeye.
Aleluya.
Injili
Mk 9: 2-10Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni