Alhamisi ya 17 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Kut 40:16-21, 34-38Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 84:2-5, 7, 10Maskani zako zapendeza kama nini, Ee Bwana wa majeshi.
Nafsi yangu imezionea shauku nyua za Bwana,
Naam, na kuzikondea,
Moyo wangu na mwili wangu
Vinamlilia Mungu aliye hai.
K. Maskani zako zapendeza kama nini, Ee Bwana wa majeshi.
Shomoro naye ameona nyumba,
Na mbayuwayu amejipatia kito,
Alipoweka makinda yake,
Kwenye madhabahu zako, Ee Bwana wa majeshi,
Mfalme wangu na Mungu wangu.
K. Maskani zako zapendeza kama nini, Ee Bwana wa majeshi.
Heri wakaao nyumbani mwako,
Wanakuhimidi daima.
Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako,
Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake.
Huendelea toka nguvu hata nguvu,
Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu.
K. Maskani zako zapendeza kama nini, Ee Bwana wa majeshi.
Hakika siku moja katika nyua zako
Ni bora kuliko siku elfu.
Ningependa kuwa bawabu
Nyumbani mwa Mungu wangu.
K. Maskani zako zapendeza kama nini, Ee Bwana wa majeshi.
Shangilio la Injili
1Pet 1:25Neno la Bwana hudumu hata milele, na neno hilo ni neno jema lililohubiriwa kwenu.
Aleluya.
Injili
Mt 13:47–53Ikawa Yesu alipoimaliza mifano hiyo, alitoka akaenda zake.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni