KUMBUKUMBU YA MT. TERESIA WA AVILA, BIKIRA NA MW
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Efe 1:15-23Kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake;ulipotenda katika kristo alipomfufua katika wafu,akamwekea mkono wake wa kuume katika ulimwngu wa roho ; juu sana katika ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani na kila jina litajwalo wala si ulimwenguni humu tu bali katika ule ujao pia akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 8:1-6Umemtawaza mwanao juu ya kazi za mikono yako
Wewe Mungu Bwana wetu,
Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni;
Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao.
K. Umemtawaza mwanao juu ya kazi za mikono yako
Nikiziangalia mbingu zako, Kazi ya vidole vyako,
Mwezi na nyota ulizoziratibisha,
Mtu ni kitu gani hat umkumbuke
Na binadamu hata umwangalie.
K. Umemtawaza mwanao juu ya kazi za mikono yako
Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu;
Umemvika taji ya utukufu na heshima
Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako
Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
K. Umemtawaza mwanao juu ya kazi za mikono yako
Shangilio la Injili
Mt 11:35Nakushukuru baba Bwana wa mbingu na nchi
Kwa kuwa mambo haya uliyaficha
Wenye hekima na akili
Ukawafunulia watoto wachanga
Aleluya.
Injili
Lk 12:8-12Na kila mtu atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali aliyemkufura Roho Mtakatifu hatasamehewa.
Na watakapowapeleka ninyi mbele ya masinagogi na maliwali na wenye mamlaka, msifadhaike kwa kuwaza maneno yenu jinsi mtakavyojibu au kusema; kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni