Jumamosi ya 30 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Flp 1:18–26Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. Ila ikiwa kuishi katika mwili, kwangu mimi ni matunda ya kazi; basi nitakalolichagua silitambui. Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo; maana ni vizuri zaidi sana; bali kudumu katika mwili kwahitajiwa zaidi kwa ajili yenu. Nami nikitumaini hayo, najua ya kuwa nitakaa na kudumu pamoja nanyi, ili mpate kuendelea na kufurahi katika Imani; hata mzidi kuona fahari katika Kirso Yesu juu yangu kwa sababu ya kuwapo kwangu pamoja nanyi tena.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 42:1–2, 4Nafsi yangu inamwonea kiu Mungu.
Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji.
Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.
K. Nafsi yangu inamwonea kiu Mungu.
Nafsi yangu inamwonea kiu Mungu, Mungu aliye hai,
Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu?
K. Nafsi yangu inamwonea kiu Mungu.
Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano,
Na kuwaongoza nyumbani kwa Mungu,
Kwa sauti ya furaha na kusifu.
K. Nafsi yangu inamwonea kiu Mungu.
Shangilio la Injili
Zab 19:8Amri ya Bwana ni safi, huyatia macho nuru.
Aleluya.
Injili
Lk 14:1, 7-11Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni