Dominika ya 13 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
2Fal 4:8-11,14-16Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 89:1-2, 15-18Fadhili za Bwana nitaziimba milele.
Fadhili za Bwana nitaziimba milele;
Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako.
Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele;
Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako.
K. Fadhili za Bwana nitaziimba milele.
Heri watu wale waijuao sauti ya shangwe,
Ee Bwana, kuenenda katika nuru ya uso wako.
Kwa jina lako hufurahi mchana kutwa,
Na kwa haki yako hutukuzwa.
K. Fadhili za Bwana nitaziimba milele.
Maana fahari ya nguvu zao ni Wewe,
Na kwa radhi yako pern be yetu itatukuka.
Maana ngao yetu ina Bwana,
Na mfalme wetu ni wake Mtakatifu wa Israeli.
K. Fadhili za Bwana nitaziimba milele.
Somo la Pili
Rum 6:3-4,8-11Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Mt 11:25Nakushukuru, Baba, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.
Aleluya.
Injili
Mt 10:37-42Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma. Ampokeave nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki. Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia. haitampotea kamwe thawabu yake.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni