Ijumaa ya Oktava ya Kuzaliwa Bwana
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
1Yn 2:29–3:6Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 98:1, 3-6Miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu.
Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
Kwa maana ametenda mambo ya ajabu.
Mkono wa kuume wake mwenyewe,
Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.
K. Miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu.
Miisho yote ya dunia imeuona,
Wokovu wa Mungu wetu,
Mshangilieni Bwana nchi yote,
Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi.
K. Miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu.
Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi,
Kwa kinubi na sauti ya zaburi.
Kwa panda na sauti ya baragumu,
Shangilieni mbele za Mfalme, Bwana.
K. Miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu.
Shangilio la Injili
Ebr 1:1-2Baada ya Mungu kusema zamani mara nyingi na kwa namna nyingi na baba zetu kwa kinywa cha manabii, siku hizi zilizo za mwisho amesema nasi kwa kinywa cha Mwana.
Aleluya.
Injili
Yn 1:29-34Tena Yohane akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye Akakaa juu yake. Wala mimi sikumjua; lakini yeye akakaa juu yake. Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu. Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni