ALHAMISI YA 2 MWAKA
· Mwaka C
Somo la Kwanza
1Sam. 18:6-9; 19:1-7Nao wale wanawake wakitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, na Daudi makumi elfu yake. Basi Sauli akagadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elf utu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme? Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile.
Kisha Sauli akasema na mwanawe Yonathani, tena na watumishi wake wote, kwamba wamwue Daudi. Lakini huyo Yonathani, mwana wake Sauli, alikuwa akipendezwa sana na DAudi. Basi Yonathani akamwambia Daudi, akasema, Sauli, baba yangu, anatafuta kukuua; basi, nakusihi, uiangalie sana asubuhi, ukae mahali pa siri na kujificha; na mimi nitatoka nje na kusimama kando ya babangu huko shambani ulipo wewe, nami nitazungumza na babangu habari zako; nami nikiona neno lolote nitakuambia.
Naye Yonathani akamsifu Daudi kwa Sauli, babaye, akamwambia, Mfalme asikose juu ya mtumishi wake, yaani, juu ya Daudi; kwa maana yeye hakukosa juu yako, tena matendo yake kwako yamekuwa mema sana. Kwa kuwa alitia uhai wake mkononi mwake, na kumpiga yule Mfilisti, naye Bwana akawatendea Israeli wote wokovu mkuu. Wewe mwenyewe uliona jambo hilo, ukafurahi; basi kwa nini kukosa juu ya damu isiyo na hatia, umwue huyo Daudi bure?
Sauli akaisikiliza sauti ya Yonathani; naye Sauli akaapa, Aishivyo Bwana, yeye hatauawa. Basi Yonathani akamwita Daudi, anye Yonathani akamjulisha mambo hayo yote. Kisha Yonathani akamleta kwa Sauli, naye alikuwa akihudhuria mbele yake, kama kwanza.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 56:1-2, 8-12 (K) 4Nimemtumaini Mungu sitaogopa.
K. Nimemtumaini Mungu sitaogopa.
Mungu, unirehemu, maana yuko atakaye kunimeza,
Mchana kutwa ananionea akileta vita.
Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa,
Maana waletao vita yangu kwa kiburi ni wengi,
Ee Mungu wangu. (K)
Umehesabu kutangatanga kwangu,
Uyatie machozi yangu katika chupa yako,
Je! Hayamo katika kitabu chako?
Ndipo adui zangu watarudi nyuma,
Siku hiyo niitapo. (K)
Neno hili najua kuwa Mungu yu upande wangu.
Kwa msaada wa Mungu nitalisifu neno lake,
Kwa msaada wa Bwana nitalisifu neno lake. (K)
Nimemtumaini Mungu,
Sitaogopa mwanadamu atanitenda nini?
Ee Mungu, nadhiri zako zi juu yangu,
Nitakutolea dhabihu za kushukuru (K)
Injili
Mk. 3:7-12Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni