Masomo ya Misa
Jumatano ya 7 ya Mwaka (Jumatano, Februari 27, 2019)
Ybs 4:11-19
Hekima huwafundisha wanawe na kuwaelimisha wanaomsikiliza. Wao wampendao hupenda uzima, nao wamtafutao watapata kibali kwa Bwana. Wao wamshikao wataurithi utukufu, hata na kudumu katika baraka ya Bwana. Wao nao wamtumikiao watamhudumia yeye aliye Mtakatifu, nao wampendao Bwana huwapenda. Amsikiaye atahukumu kwa kweli, naye amjalie atakaa katika chumba chake cha ndani. Akimtumaini atamrithi, atakuwa naye hata vizazi vyote vya milele. Kwa maana mwanzo Hekima ataandamana naye kwa njia za kikombo, na kumletea hofu na woga, na kumwadhibisha kwa marudi yake, hata atakapoweza kumwamini roho yake, na kumhakiki kwa hukumu zake. Ndipo atakaporudi na kumuongoza moja kwa moja, na kumfurahisha, na kumfunulia siri zake. Walakini akipotea, Hekima atamwacha na kumtia mikononi mwa maangamizi
Zab 119:165, 168,171-172, 174-175
Wana amani nyingi waipendao sheria yako,
Wala hawana la kuwakwaza.
(K) Wana amani nyingi, ee Bwana, waipendao sheria yako.
Nimeyashika mausia yako na shuhuda zako,
Maana njia zangu zote zi mbele zako.
(K) Wana amani nyingi, ee Bwana, waipendao sheria yako.
Midomo yangu na itoe sifa,
Kwa kuwa unanifundisha mausia yako.
(K) Wana amani nyingi, ee Bwana, waipendao sheria yako.
Ulimi wangu na uiimbe ahadi yako,
Maana maagizo yako yote ni ya haki.
(K) Wana amani nyingi, ee Bwana, waipendao sheria yako.
Ee Bwana, nimeutamani wokovu wako,
Na sheria yako ndiyo furaha yangu.
(K) Wana amani nyingi, ee Bwana, waipendao sheria yako.
Nafsi yangu na iishi, ipate kukusifu,
Na hukumu zako zinisaidie.
(K) Wana amani nyingi, ee Bwana, waipendao sheria yako.
Zab. 119:28, 33
Aleluya, aleluya,
Unitie nguvu sawasawa na neno lako, Ee Bwana, unifundihse njia ya amri zako.
Aleluya.
Mk 9:38-40
Yohane alimjibu Yesu, akamwambia, Mwalimu, tulimwona mtu akitoa pepo kwa jina lako, ambaye hafuatani nasi; tukamkataza, kwa sababu hafuatani nasi. Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu akaweza mara kuninenea mabaya; kwa sababu asiye kinyume chetu, yu upande wetu.
Maoni
Ingia utoe maoni