Jumamosi ya 34 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Ufu. 22:1 – 7Kisha akaniambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu war oho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi. Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 95:1 – 7Maranatha, Uje, Bwana Yesu.
Njoni tumwimbie Bwana,
Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.
Tuje mbele zake kwa shukrani,
Tumfanyie shangwe kwa zaburi.
K. Maranatha, Uje, Bwana Yesu.
Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu,
Na mfalme mkuu juu ya miungu yote.
Mkononi mwake zimo bonde za dunia.
Hata vilele vya milima ni vyake.
Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya,
Na mikono yake iliiumba nchi kavu.
K. Maranatha, Uje, Bwana Yesu.
Njoni, tuabudu, tusujudu,
Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba.
Kwa maana ndiye Mungu wetu,
Na sisi tu watu wa malisho yake,
Na kondoo za mkono wake.
K. Maranatha, Uje, Bwana Yesu.
Shangilio la Injili
Zab. 119:135Umwangazie mtumishi wako uso wako, na kunifundisha amri zako.
Aleluya.
Injili
Lk. 21:34-36Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni