Alhamisi ya 32 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Flm. 7 – 20Kwa hiyo, nijapokuwa nina ujasiri katika Kristo kukuagiza likupasako; lakini, kwa ajili ya upendo nakusihi, kwa kuwa ni kama nilivyo, Paulo mzee, na sasa mfungwa wa Kristo Yesu pia. Nakusihi kwa ajili ya mtoto wangu niliyemzaa katika vifungo vyangu, yaani, Onesimo; ambaye zamani alikuwa hakufai, bali sasa akufaa sana, wewe na mimi pia; niliyemtuma kwako, yeye mwenyewe, maana ni moy wangu hasa; ambaye mimi nalitaka akae kwangu, apate kunitumikia badala yako katika vifungo vya Injili.
Lakini sikutaka kutenda neno lolote isipokuwa kwa shauri lako, ili kwamba wema wako usiwe kama kwa lazima, bali kwa hiari. Maana, labda ndiyo sababu alitengwa nawe kwa muda, ili uwe naye tena milele; tokea sasa, si kama mtumwa, bali zaidi ya mtumwa, ndugu mpendwa; kwangu mimi sana, na kwako wewe zaidi sana, katika mwili na katika Bwana. Basi kama ukiniona mimi kuwa mshirika nawe, mpokee huyu kama mimi mwenyewe. Na kama amekudhulumu, au unamwia kitu, ukiandike ndicho juu yangu. Mimi Paulo nimeandika kwa mkono wangu mwenyewe, mimi nitalipa. Sikuambii kwamba nakuwia hata nafsi yako. Naam, ndugu yangu, nipate faida kwako katika Bwana; uniburudishe moyo wangu katika Kristo
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 146:7 – 10Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake.
Bwana huishika kweli milele,
Huwafanyia hukumu walioonewa,
Huwapa wenye njaa chakula,
Hufungua waliofungwa.
K. Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake.
Bwana huwafumbua macho walopofuka,
Bwana huwainua walioinama,
Bwana huwapenda wenye haki,
Huwahifadhi wageni.
K. Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake.
Huwategemeza yatima na mjane,
Bali njia ya wasio haki huipotosha.
Bwana atamiliki milele,
Mungu wako, Ee Sayuni, kizazi hata kizazi.
Aleluya.
K. Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake.
Shangilio la Injili
Zab. 27:11Ee Bwana, uifundishe njia yako, na kuniongoza katika njia iliyonyoka.
Aleluya.
Injili
Lk. 17:20-25Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni