Visakramenti katika Kanisa Katoliki
6 Septemba 2018 · na Shajara Administrator
Ni alama takatifu ambazo kwa sababu zinafanana na Sakramenti, zinaashiria kupatikana kwa matunda ya kiroho kupitia maombi ya kanisa. Visakramenti huwasaidia watu kupokea tunda la msingi la Sakramenti na mazingira mbalimbali ya maisha hutakaswa.
Katika maana nyengine: Visakramenti ni shara takatifu zilizoanzishwa na Kanisa ambazo lengo lake ni kuwaandaa watu kupokea tunda la Sakramenti na kutakatifuza mazingira mbalimbali ya maisha.
Mfano wa Visakramenti: Misalaba, Medani, Rozari, Skapulari, Maji ya baraka, Matawi yaliyobarikiwa, Majivu yaliyobarikiwa n.k
Visakramenti hufanyikaje?
Visakramenti hufanyika kwa njia ya Baraka. Ukiwa na Msalaba, Rozari Skapurari etc ambayo haijabarikiwa ni kazi bure haiweizi kufanya kazi yoyote. Ni baada ya kubarikiwa na Padre ndipo Visakramenti hupata pumzi ya uhai ndani yake. Hivyo twasema ni katika kubarikiwa Visakramenti hufanya hai navyo huweza kutubariki.
NB: Kila Mkristo mbatiwa naye alibarikiwa hivyo huitwa "baraka". Wabatizwa wote tumebarikiwa na Mungu baraka za rohoni katika ulimwengu wa roho na ndani yake Kristo (Waefeso 1:3). Hivyo walei huweza kusimamia baadhi ya baraka kulingana na utaratibu wa Kanisa. Walei hawatasimamia baraka ambazo usimamizi wake umetegwa maalumu kwa ajili ya huduma ya Daraja (Maaskofu, Mapadre au Mashemasi)
Kazi ya Visakramenti ni nini?
Visakramenti vinatutayarisha kupokea neema na pia kushirikiana nayo. Tofauti na Sakaramenti ambazo zenyewe hutoa neema. Hivyo huchota visakramenti nguvu kutoka katika Sakramenti. Chukua mfano wa Visakramenti tajwa hapo juu na angalia kazi yake, mfano Maji ya baraka au Rozari. Tafakari namna ambavyo Visakramenti vilivyobarikiwa vinavyotupa nafasi ya kuishi ukatoliki wetu. Kwa uchache Visakramenti hutusaidia;
Kusali
Kufakari imani yetu
Kupunga pepo wabaya (uwingaji)
Kupokea baraka mbalimbali
Kutukinga na hatari za kimwili na kiroho
Kubariki watu na vitu nakadalika
Kuna kazi na faida nyingi tuzipatazo kutoka katika Visakramenti. Visakamenti ni mto wenye baraka tele ambao tunaweza kujichotea baraka tukienda na vyombo visafi.
Matumizi sahihi ya Visakramenti
Kuvaa
Visakramenti vimebarikiwa, hivyo ndani yake vimebeba baraka, ni muhimu vitumike kwa heshima kubwa sana. Ni busara kuvivaa wakati wote lakini si katika mazingira kama kumbi za starehe au disko au katika matendo ya uovu. Wawezaje kutenda dhambi huku umevaa Rozari au Skapulari?
Kuvitunza
Visakramenti kama Msalaba, Picha za watakatifu au maji ya baraka vihifadhiwe katika mahali pasafi na pa kupendeza, si vizuri kuvichnganya na vitu vengine. Maana hivi ni Vibarikiwa basi vituzwe kama vibarikiwa.
Kusali
Hatuvai Visakramenti kama hirizi, tunahitaji vitusaidie kufikia Sakramenti mbalimbali. Tunapaswa kuvitumia katika sala sio kuviacha kama ulinzi tu, kama ni Rozari hakikisha unasali, kama ni msalaba upe heshima inayostahili.
Visakaramenti Vimeharibika Umbo/Unataka kuvitupa?
Visakramenti vyaweza kuharibika katika hali yake ya umbo, mfano Rozari imekatika, Picha imeungua nusu au msalaba umevunjika upande. Au ulikua na msalaba mdogo sasa umeninua mkubwa unataka kuutupa, je ni sahihi?
Tukumbuke visakramenti hufanyika katika ngazi mbili, kwanza umbo la halifi tunaloliona na pili Kubarikiwa kwake kunakofanya kuwa kisakramenti. Baraka huwa katika umbo zima si sehemu tu, hivyo kuharibika kwa umbo hakutoi baraka iliyomo ndani yake.
Visakramenti vinapoharibika twapaswa kuendelea kuvitunza kwa heshima kuu kama ambavyo tumevitunza kutoka awali. Kuvitupa au kuviharibu hii huwa ni kufuru kwa baraka iliyomo katika visakramenti. Kama hutaweza kuvitunza ni bora kuvipeleka kanisani nao watajua namna ya kuvihifahdi. VISAKRAMENTI HAVITUPWI.
Maoni (14)
edwin msekalile · 10 Septemba 2020
asante kwa mafundisho
Papy LWANGA MULINDWA · 5 Agosti 2021
Shukrani
Erick Liwa · 20 Julai 2022
makala kama hizi zinabidi zipelekwe kwa watu wengi zaidi.
Donata Musa · 7 Julai 2026
Kwel
STANISLAUS PANGA · 15 Julai 2026
Cw uwe na xiku njema
Julius Materu · 7 Novemba 2022
Imekaa vizuri sana nitawamegea na wenzangu tukisali jumuia.
Moses Liaram · 12 Oktoba 2026
Tumsifu yesu
Joshua Paschal · 3 Mei 2023
Asante kwa elimu mana nimepata kujua nini maana ya sakramenti
Martin Mzopola · 6 Juni 2026
Najibu kutokana na katekisim ndogo ya mosho. Sakaramenti ni alama wa iliyowekwa na yesu kristo ili kutupatia neema ya namasitahili ya kufika mbinguni tukizipokea vyema.
Moses Liaram · 12 Oktoba 2026
Tumsifu yesu kristo
Erick Galus · 24 Agosti 2023
Kwnn tuna sali rozali
STANISLAUS PANGA · 15 Julai 2026
Kila kitu ni imani imani yako ndy itaku saidia Erick
VICENT MDUMULA · 22 Septemba 2023
ASANTE
STANISLAUS PANGA · 15 Julai 2026
VISENT UKO POW
Emmanuel Erot · 16 Desemba 2023
Naomba nifunzeni kusali rozari
Emmanuel Erot · 16 Desemba 2023
Naomba nifunzeni kusali rozari
LUCAS KAFUMU · 14 Desemba 2024
Nipigie simu kama haujui kusali lozari nikufundishe maana wote ni wa kristo kwa namba 0718884911 au 0752532690 mungu awabariki wote
PETER PANGA · 17 Julai 2026
NIPIGIYE KWENYE NAMB ZANGU 0663504000 AU 0638444573 KWA USHAURI
PETER PANGA · 17 Julai 2026
0663504000
Rose Chuwa · 8 Aprili 2025
somo zuri sana naomba somo zaidi
Donata Musa · 7 Julai 2026
Mapendo
STANISLAUS PANGA · 15 Julai 2026
JAMAN
Fedi ibrahimu ibrahimu · 10 Oktoba 2026
Tuwe tunasali rozari takatifu inasaidia katika maisha ya mkristo
Fedi ibrahimu ibrahimu · 10 Oktoba 2026
Kweli
Fedi ibrahimu ibrahimu · 10 Oktoba 2026
Daimaa
Esther Moshy · 12 Oktoba 2026
asante Kwa Somo zuri