Ijumaa. 03 Mei. 2024

Mt. Damas wa Kwanza , Papa

Damas wa Kwanza , Papa

Damasi alizaliwa mwaka 305 katika familia ya Kihispania. Alikuja Roma (Italia) pamoja na jamaa yake, akapadirishwa, na katika mwaka 366 wakati wa matatizo mengi sana aliteuliwa kuwa Papa. Aliitisha mikutano mingi ili kuwapinga wazushi walioleta mifarakano katika Kanisa. Papa huyu ndiye aliyemweka Mt. Jeronimo kama mwandishi wake, akimshauri kutafsiri Maandiko Matakatifu (tazama 30 Septemba). Alitangaza pia amri ya kuimba zaburi katika makanisa yote wakiitikia zamu kwa zamu, na mwisho wa kila zaburi waimbe: " Atukuzwe Baba, na Mwana, na Roho Mtalatifu". Na ndiye aliyeanza desturi ya kuimba Aleluya wakati wa Pasaka.

Pia aliandika kitabu, akatumia mashairi kwa kuusifu uzuri wa ubikira. Mtakatifu Jeronimo humtaja kama mtu bora, asiye na mfano, Mwalimu wa Maandiko Matakatifu. Papa Damasi alihimiza sana ibada kwa wafiadini, akayapamba makaburi yao kwa kuyabuni maneno kutoka maandiko matakatifu. Alikufa mwaka 384.

Maoni


Ingia utoe maoni