Jumanne. 16 Julai. 2024

Mt. Anthony wa Padua

Anthony wa Padua

Mt Anthony wa Padua alizaliwa mwaka 1195 huko Lisbon,Ureno.Aliitwa Fernando Martins.Alizaliwa katika familia njema yenye uwezo.Akiwa na umri wa miaka 15,aliomba kupelekwa seminari ya Santa Cruz katika mji wa Coimbra,ambako alisoma teolojia na kilatini.Akapata daraja la upadre,na akawa hapo hapo mjini Coimbra.Wakaja Wa franciscan ambao walitengeneza makao yao nje ya mji.Padre Fernando Martin akawapenda,akaomba ruhusa ili ajiunge nao.Aliporuhusiwa akajiunga nao, akabadili jina,akaitwa Anthony.

Akasafiri mpaka Morocco,kueneza neno la Mungu.Huko akaugua sana,ikabidi arudishwe Coimbra kwa matibabu.Chombo alichopanda kilivunjika kwa dhoruba,hata hivyo mt Anthony alifika Sicily, na akapelekwa katika mji wa Tuscany ili apate matibabu na mapumziko.Wakati akiendelea na matibabu,alitumia muda wake mwingi akisali na kusoma.Muda huo pia walipata wageni ambao walikuwa Wa Dominican. Kukawa na hali ya kutegemea kila upande kutoa mahubiri.Mkuu wa Wa franciscan alimwambia Mt Anthony atoe mahubiri kadiri Roho Mtakatifu atakavyomjaalia.Akatoa mahubiri yaliyowagusa wote,na kuwasisimua mno.Habari za mahubiri hayo zikamfikia Mt Francis wa Assisi,ambaye alipomuona Mt Anthony wakawa marafiki.Mt Anthony alikuwa na kitabu cha zaburi,ambacho ndani yake kulikuwa na mafundisho ya ufafanuzi kwa wanafunzi.Kitabu hicho kwake kilikuwa kitu chenye thamani mno.Mwanafunzi mmoja aliamua kutoroka seminarini,akaiba na kitabu hicho.Mt Anthony alisali akiomba kitabu hicho kipatikane na kirudi kwake.Lakini yule aliyekiiba alirudi nacho,akamrudishia.Kitabu hicho kimehifadhiwa katika kanisa la Bologna hata sasa.

Mt Anthony aliendelea na kuhubiri na kufundisha katika miji mbalimbali Ufaransa na Italia.Kuna wakati aliamua kwenda mtoni,akahubiria samaki baada ya watu kukosa kusikiliza mahubiri yake.Watu walivyogundua utulivu na usikivu wa samaki nao wakakusanyika na kusikiliza. Mt Anthony alikufa mwaka 1231.Akatangazwa Mtakatifu Sikh 336 baada ya kifo chake na Papa Gregory IX.Mwaka 1946 Papa Pius XII alimtangaza Mt Anthony kuwa Daktari wa kanisa.

Maoni


Ingia utoe maoni