Margareta Maria Alakok, Mtawa
Kule Ufaransa katika karne ya 17, upendo kwa Mungu ulikuwa umepooza sana. Watu wengi waliuacha mwenendo wa kikirstu na wengine waliukubali uzushi wa Jansenio aliyehubiri kwamba Mungu hawapendi watu wote sawa, bali anawapenda wengine, na baadhi yao anawaacha kabisa. Ili kuwaamshia wakatoliki upendo kwa Mungu, watakatifu watatu hasa walioishi kati ya miaka 1625 na 1690, walliieneza, kwa bidii sana, ibada kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu, nao ni Mt. Yohani Eudes (1610-1680).Margareta Maria alizaliwa katika nchi ya Ufaransa mwaka 1647.Baada ya kifo cha baba yake, wakamwingiza katika shule ya shirika la Mt. Klara. Alipokuwa na umri wa miaka kumi na mmoja alishikwa na ugonjwa na kwa sababu hiyo hakuweza kutembea kwa muda wa miaka minne. Kisha kupona, alianza kuzipendelea anasa za ulimwengu, kwa kuvaa kimalidadi. Bwana wetu alimtokea akamwambia. Ukiniacha mimi na kutaka mchumba mwingine, mimi nitakuacha kwa siku zote. Margareta alisikiliza mashauri ya Yesu na alipokuwa na umri wa miaka ishirini na miwili, akaingia katika shirika la masista wa Maonano (Visitation Sisters) huku Paray-le-Monial (Ufaransa).Mwaka 1673, alipokuwa akisali mbele ya Saktramenti Kuu Bwana Yesu alimtokea akamwonyesha moyo wake akisema: “Tazama moyo wangu unaowaka mapendo kwa watu.Ningetaka kuwafumbulia watu moyo wangu, na kuwagawia neema zote zilizomo. Siku nyingine, Mwokozi alimtokea akamwonyesha vidonda vitano mwilini mwaka akisema: nimewapenda watu kwa mapendo makubwa. Lakini watu hawana shukrani. Laiti watu wengi wangeyafikia mapendo yangu, ningekuwa tayari kufanya zaidi, na kufanya bado zaidi kwa ajili yao. Lakini watu wanaonionyesha ubaridi na ugumu wao. Ewe mwanangu, unifurahishe kidogo pahali pa wakosefu hao.Mwezi Juni mwaka 1675, Bwana wetu alimwonyesha tena moyo wake akisema: “Ndio moyo huu unaopenda sana watu, na watu hawaupendi.
Maoni
Ingia utoe maoni